У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY-THE SCHOOL OF HEALING 18/03/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY-THE SCHOOL OF HEALING 18/03/2026 MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 25 MADA: "KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON) NENO KUU: Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; UJUMBE WA LEO: KUTOKA MSIMU MPAKA HATMA KWA NJIA YA SADAKA Mhubiri 3 : 1 1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3 : 19 19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; Kutoka Benoni mpaka Benjamin ( Mbwa-mwitu mwenye mawindo). SADAKA NA MAOMBI KAMA KIBEBEO CHA MSIMU MPYA WA UZAO WANGU. Sadaka na Maombi vina tabia ya kuondoa zuio kwenye Ulimwengu wa roho na kuvunja mipaka iliyowekwa. Kumbukumbu 23 : 5 Sadaka na Maombi vina tabia ya kufufua vilivyokufa na kuweka uhai ndani yake. Mfano dokasi na mwanamke Mshunami. Matendo 9 : 36 - 40 36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. Zaburi 20 : 14 Sadaka na Maombi vina uwezo wa kubadilisha Watu Uelekeo na Kitabia Hesabu 25 : 1 - 3 1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. Sadaka ina tabia ya Kuvuruga Kanuni za ulimwengu wa roho juu ya Eneo na watu wanaokaa juu yake. Mwanzo 22 : 2 2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. Ezra 9 : 4 4 Ndipo wakanikusanyikia watu wote walioyatetemekea maneno ya Mungu wa Israeli, kwa sababu ya lile kosa la watu wa uhamisho; nami nikaketi kwa mshangao hata wakati wa sadaka ya jioni. Mithali 7 : 14 14 Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Sadaka huwa ina tabia ya Kuvuruga fikra na Kutengeneza fikra mpya kwa wahusika. 1 Wafalme 18 : 37 - 40 37 Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. 38 Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. 39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. 40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko. Zaburi 49 : 3 3 Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara. 2 Wakorintho 11 : 3 3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka. 2 Wafalme 4 : 24 24 Akatandika punda, akamwambia mtumishi wake, Mwendeshe, twendelee mbele. Usinipunguzie mwendo, nisipokuambia. 25 Basi akaenda, akafika kwa yule mtu wa Mungu, katika mlima wa Karmeli. Ikawa, yule mtu wa Mungu alipomwona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, Tazama, Mshunami yule kule. 26 Tafadhali piga mbio sasa kwenda kumlaki, ukamwambie, Hujambo? Mume wako hajambo? Mtoto hajambo? Akajibu, Hawajambo. 2 Wafalme 4 : 33 - 36 Mhubiri: Mwl. James Kamera Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com Mhubiri: Mwl. James Kamera Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com