У нас вы можете посмотреть бесплатно Waziri Mkuu kufanya ziara Arusha или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Arusha kuanzia Februari 22 hadi 24, 2026, ambapo atakagua miradi sita yenye thamani ya Shilingi bilioni 194.2 katika wilaya za Arumeru, Longido na Arusha, pamoja na kuzungumza na wananchi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, siku ya kwanza ya ziara hiyo itahusisha uwekaji jiwe la msingi katika bweni la kisasa la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sayansi cha Nelson Mandela, ukaguzi wa upanuzi wa miundombinu ya Hospitali ya Oltrumet na mkutano wa hadhara Ngaramtoni. Februari 23, Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Wilaya ya Longido ambako atapokea taarifa ya mradi wa maji Sinya, kuzindua upanuzi wa Shule ya Sekondari Sinya hadi kidato cha tano na sita, kukagua Kituo cha Huduma za Pamoja (One Stop Border Post) Namanga na kuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Msingi Namanga. Siku ya mwisho ya ziara hiyo, Waziri Mkuu atakuwa Wilaya ya Arusha akitarajiwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Bondeni City, kuweka jiwe la msingi katika soko la Kilombero na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara jijini Arusha. Mkuu wa Mkoa amewaalika wananchi kushiriki katika mikutano hiyo ya hadhara, akieleza kuwa ziara hiyo inalenga kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza maoni ya wananchi katika maeneo husika.