У нас вы можете посмотреть бесплатно Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Historia ya Ukombozi Kusini Mwa Afrika kwa Familia ya Mbita или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kituo kimefanya hafla fupi ya kuikabidhi familia ya aliyekuwa Mwanaharakati na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi wa Afrika, Hayati Brig. Jenerali Hashim Mbita, Juzuu ya vitabu vya Mradi wa SADC (Hashim Mbita Project) ikiwa ni kuenzi mchango mkubwa uliotolewa na Marehemu Mbita wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Mawaziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Maliasili na Utalii, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Makabidhianao hayo yalifanywa na Mratibu wa Kituo cha Ukombozi wa Bara la Afrika Ndg. Boniface Kadili kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Ofisi za Kituo cha Ukombozi kilichopo Jijini Dar es Salaam. Familia imetoa shukrani kwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa heshima ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kumuenzi mpendwa wao.