У нас вы можете посмотреть бесплатно NAIBU WAZIRI ELIMU WANU ONGEZENI KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU DIT MWANZA IKAMILIKE KWA WAKATI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
NAIBU WAZIRI ELIMU WANU ONGEZENI KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU DIT MWANZA IKAMILIKE KWA WAKATI Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amemtaka Mkandarasi wa COMFIX & ENGINEERING kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano Afika Mashariki katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza, ili ikamilike kwa wakati kulingana na maktaba. Ametoa maagizo hayo Leo jijini Mwanza wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo huku akiwataka wazabuni wote kuhakikisha vifaa na mitambo vinawasili na kufungwa kwa wakati ili kuwezesha utoaji wa mafunzo kwa wakati Mhe. Wanu Ameir amesema ucheleweshaji wa ujenzi unaweza kuathiri malengo ya Serikali ya kuhakikisha vijana wanapata ujuzi na umahiri unaohitajika katika soko la ajira la ndani na kimataifa, kama alivyoelekeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa upande Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa katika Kampasi ya DIT Mwanza kinajengwa Kituo cha Kikanda cha Umahiri cha uchakataji na utengenezaji wa bidhaa za Ngozi ambacho kinatekelezwa kupitia Mradi wa EASTRIP. Amesema kuwa ujenzi huo unahusisha majengo matano ambayo ni jengo la kufundishia, jengo la taaluma, hosteli mbili na karakana ya kisasa kwa ajili ya mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam (DIT) Kampasi ya MWANZA Dkt. John Msumba amesema kuwa Kampasi hiyo imefufua Sekta ambayo ilikuwa imekufa nchini kutokana na kukosekana Kwa wataalamu na kwamba Viwanda Kwa sasa vinapata wataalamu tofauti na awali ambapo walikuwa wakilazimika kuwatoa nje ya nchi.