У нас вы можете посмотреть бесплатно KALIMA YA SHEIKH SALIM BARAHIYAAN - CHUO CHA UALIMU ARAFAH NI MFANO WA KUIGWA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KALIMA YA SHEIKH SALIM BARAHIYAAN - CHUO CHA UALIMU ARAFAH NI MFANO WA KUIGWA. Mudir Markaz Kuu wa Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Centre (AMYC), Sheikh Salim Barahiyan, amepongeza Chuo cha Ualimu Arafah kwa kuzalisha walimu mahiri na wenye nidhamu, na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo vya kuigwa nchini. Akizungumza leo Novemba 22, kwenye mahafali ya wahitimu wa mwaka 2025, Sheikh Barahiyan amesema chuo hicho kimeendelea kuipa heshima AMYC kutokana na walimu wake kuonesha uwezo mkubwa katika ufundishaji na maadili ya kazi. Amefafanua kuwa mara kwa mara amekuwa akipokea pongezi kutoka maeneo mbalimbali, ikiwemo idara za serikali. Miongoni mwa pongezi hizo ni kutoka kwa Msimamizi wa Elimu Kanda ya Kaskazini, ambaye amesema umahiri wa walimu wanaozalishwa na chuo hicho umeendelea kurahisisha kazi kwa watendaji wa elimu kutokana na nidhamu yao pamoja na kiwango cha juu cha taaluma wanachokionesha. Katika salamu zake kwa wahitimu, Sheikh Barahiyan amewahimiza kuongeza elimu ili waendane na mabadiliko ya sifa za ajira, akieleza kuwa ajira nyingi katika sekta ya elimu, hususan mashuleni, sasa zinahitaji kiwango cha kuanzia Diploma. #redioihsaanfm102.1 #mawasilianomarkazkuu #ansaarmuslimyouthcentre