У нас вы можете посмотреть бесплатно SHINYANGA SASA NI SHWAAA...BOMBADIER KUANZA KUTUA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk Charles Msonde amesema ujenzi wa kiwanja cha ndege Shinyanga umefikia asilimia 75 na utakamilika Juni 10, mwaka huu. Amesema kukamilika kwake kutawezesha ndege aina ya Bombadier Q400 kuanza kukitumia kiwanja hicho chenye urefu wa mita 2200 na upana wa mita 30 kilichogharimu Sh48.5 bilioni. Akizungumza leo Machi 20, 2025 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), iliyokagua maendeleo ya ujenzi huo, Dk Msonde amesema njia za kuruka na kutua ndege, maegesho na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani zimekamilika. "Kilichobaki ni jengo la abiria ambalo ujenzi wake upo kwenye hatua ya mwisho kukamilika," amesema. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustine Vuma Holle ameiagiza wizara ya ujenzi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati. Amesema hatua ambayo umefikia ni nzuri, akiipongeza wizara ya ujenzi na Wakala wa Barabara (Tanroads), kwa kazi nzuri na kuwahimiza kumsimamia mkandarasi ili asilimia 25 iliyobaki ikamilike kwa wakati na huduma kiwanjani hapo zianze. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Julius Mtatiro amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja hicho kutaondoa adha kwa watumiaji wa huduma za ndege na kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye mkoa huo.