У нас вы можете посмотреть бесплатно MBUNGE BULAYA AWATAKA WANANCHI WA NYATWALI KUTULIA: HAKUNA MAELEKEZO YA KUONDOLEWA KWAO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mheshimiwa Ester Bulaya, amewataka wananchi waliobaki katika eneo la Nyatwali kuendelea kuwa watulivu na kutoingiwa na hofu, akisisitiza kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hajatoa maelekezo yoyote ya kuondolewa kwa wananchi hao kwa sasa. Kauli hiyo inakuja kufuatia tukio lililotokea jana, tarehe 2 Februari 2026, ambapo iliripotiwa kuonekana kwa askari katika eneo la Nyatwali wakiwataka baadhi ya wananchi kuondoka, hali iliyozua sintofahamu, hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya wananchi bado hawajalipwa fidia zao stahiki. Mheshimiwa Bulaya amesisitiza kuwa haki za wananchi lazima ziheshimiwe, na hakuna mwananchi anayepaswa kuondolewa au kuathiriwa bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo ulipaji wa fidia kwa wale wanaostahili. Mbunge Bulaya ameyasema haya alipokuwa akichangia mjadala wa Mpango Elekezi wa Maendeleo ya Taifa wa Muda Mrefu wa mwaka 2026/2027 hadi 2050/2051 (DIRA).