У нас вы можете посмотреть бесплатно MALIPO YA KODI YA PANGO LA ARDHI KWA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI INAKULETEA UTARATIBU MPYA UTAKAO KURAHISISHIA KUJUA UNADAIWA KIASI GANI CHA KODI YA PANGO LA ARDHI NA KULIPIA KWA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI • Bonyeza *152*00# • kisha Chagua namba 4 - MALIPO YA SERIKALI • Chagua namba 2 - KUKADIRIA KODI YA KIWANJA • Kisha chagua 1 kama kiwanja chako kipo Dar es salaam na 2 kama kiwanja chako kipo mikoa mingine. • Kisha weka namba 1 Kuweka namba ya Hati au namba 2 kuweka ID ya kiwanja. • Kisha Ingiza namba husika • Na Subiri ujumbe mfupi wenye namba ya kulipia inayoanzia na 99117 na uinakili. UNAWEZA KUJUA UNADAIWA KIASI GANI KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI WA MAANDISHI YAANI SMS • Fungua sehemu ya kuandikia ujumbe mfupi wa maandishi yaani (SMS) • Andika neno HATI au neno ID • Ikifuatiwa na NAMBA YA HATI au NAMBA YA ID • Kisha andika 1 kwa viwanja vya Dar es salaam na 2 kwa viwanja vya Mikoa mingine. • Mfano kama namba ya hati ni 12345 na ipo Dar es salaam. Utaandika HATI 12345 1 • Tuma kwenda namba 15200 • Kisha subiri SMS yenye namba za kulipia inayoanzia na 99117 na uinakili. • Au tembelea tovuti ya Wizara www.ardhi.go.tz na bofya menu ya KADIRIA KODI YA ARDHI na fuata maelekezo. SASA UNAWEZA KULIPIA KWA NJIA YA MPESA AU TIGO PESA • Kwa Mpesa Ingia LIPA KWA M-PESA, kwa tigopesa ingia LIPIA BILI. • Kisha weka namba ya kampuni ambayo ni 888999 ikifuatiwa na namba ya kumbukumbu uliyoinakili. • Aidha unaweza kulipia tawi lolote la benki ya NMB na CRDB. • Na utatumiwa stakabadhi yako kwa njia ya SMS au fika kituo chochote cha malipo ya kodi ya pango la ardhi ukiwa na uthibitisho wa malipo yako ili kupata stakabadhi. • Kwa maelezo zaidi au tatizo lolote piga namba +255222121107