У нас вы можете посмотреть бесплатно Ferooz ft. Juma Nature - Bosi (Official Video) или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
LYRICS [Verse 1: Ferooz] Homa kali imenichachamaa mwilini Watoto wiki ya pili wamefukuzwa ada shuleni Na mtaani sina amani nimeandamwa na madeni Mama watoto wahi kazini kwangu upate taarifa Kama kuna msaada wowote bosi anaweza kupa aaaaaah Alfajiri iliofuata Mama akajidamka Tukaagana vizuri, kazini kwangu akaibuka Kufika pale bila ya kuipoteza mida Akaingia ofisini na kuanza kueleza shida Okay okay Bosi akamkubalia Na fedha akampatia, Kumbe tayari alikuwa ameshamzimia Ili kumkoleza, fedha akamuongeza Katika maongezi maongezi boss akamtongoza Mama akiangalia hali aliyoiacha nyumbani Ni dhiki kubwa ambayo kwakweli hakuitamani Na kama unavyoelewa mapenzi ya sikuhizi Alisha ahidiwa atagharamiwa yote matumizi Ikibidi akubali tena bila kipingamizi Baada ya kupita kipindi mapenzi yakaanza Shamiri Huku kabwela mimi sina hile wala hili Bosi akaanza kunipa safari nyingi za kikazi Ili nikiondoka apate nafasi ya kumwaga radhi Hadi kufika hapo mi sikuelewa kama kuna picha ninayochezewa Wafanyakazi wenzangu wakaja nishtua Kwamba sikuhizi wife wako bosi anamchukua Kwakuwa nilimuamini sana wife nilibisha Lakini baada ya kuchunguza nikaja hakikisha Nikamwambia mama watoto ila akakataa Nikimueleza bwana mkubwa itakuwa kizaa zaa, Itakuwa kizaa zaa [Chorus: Ferooz] Wanasema sikubali bora niangamie Wengine wanasema heri nivumilie Kwengine wapi ntapata ajira nambie Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie Watoto wataishi kwenye yapi mazingira Nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira [Verse 2] Taswira yangu ilipoanza kukosa mwangaza Na Afya ikaanza dhohofika kwaajili ya kuwaza Hata muda mrefu hauchukua, nikazidi kuchanganyikiwa nilivyogundua Nilivyogundua kwamba, Laazizi wangu waridi la maisha amebeba mimba kwenye mazingira yalionitatanisha Jiujezi mbwiga aliekosa wazazi, nikashindwa kula wala kupata usingizi Nikawa nakesha, nikimuomba manani anijalie muelekeo Huku nikivuta subra kusubiri matokeo Dah Ila sikuamini yangu macho, ilipofika kipindi ambacho Wife wangu alipojifungua ujauzito Kuzaliwa mtoto kafanana na yule kizito Akili ikanituma nichukue panga au rungu Ili niende kumdhuru yule mtoto kwa uchungu Nahisi malaika wakapooza jazba zangu Na kunikumbusha kuwa kile ni kiumbe cha Mungu Baada ya kupita siku tatu wakaja wafanyakazi Wenzangu Eti kunipa pongezi wakiwa na yule bosi wangu Machungu yalinijaa moyoni, lakini nilishindwa nifanye nini Nikimuharibia bosi ntafukuzwa kazini Wadhifa wake wafanya apate ninyanyasa Nami kuishi hivyo nafsi yangu inakataa Nachohofia endapo kazi nitaikosa Watoto wataishi vipi naomba ushauri wa kufuata Mwenzenu mimi, mwenzenu mimi [Chorus: Ferooz] Wanasema sikubali bora niangamie Wengine wanasema heri nivumilie Kwengine wapi ntapata ajira nambie Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie Watoto wataishi kwenye yapi mazingira Nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira Wanasema sikubali bora niangamie Wengine wanasema heri nivumilie Kwengine wapi ntapata ajira nambie Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie Watoto wataishi kwenye yapi mazingira Nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira [Verse 3: Juma nature] We feruzi muharibie, muharibie uyo, mkate kidevu Boss mkurugenzi kitambi meneja Usione tumekonda ukadhania mateja Sasa ndo umemfanya nini mfanyakazi mwenzetu? Si umemchukulia mkewe ndoman analalamika Au kuna jingine Ferooz hataki kuwajibika Sikiliza mwanangu feruzi, hapa hatoki mtu Ukisema umuache utakuwa umeidhulumu nafsi Yani najiskia vibaya kwanini huyu bosi hafi Ananiudhi Feruzi mharibie, mbona unasita sita? Feruzi mkate kidevu mzee, Au unamuogopa? [Ferooz] Naweza, Hivyo naweza, ninachohofia familia kuiteketeza Nyumba ninayokaa ni mali ya shirika Nitaenda ishi wapi bosi akikasirika? Ukoo mzima mimi unanitegemea, na mimi kazini pale ndo nilipoegemea Kutokana na unyama bosi alionitendea Wengine wanashauri hata kwa mganga ningemwendea [ferooz] Ooooh oooh hapana, hapana, hapana Hivyo ndo utaharibu kabisa, hivyo ndo utaharibu kabisa Nishaishi vipi kama mtumwa anaekosa Uhuru Akati mie hali hio binafsi inanidhuru Kitu kinachoniongeza mimi machungu Kubambikiwa mtoto ambae si damu yangu Eeeh mola nisaidie Nipo kwenye janga la utata, nipo kwenye janga la utata [Chorus: Ferooz] Wanasema sikubali bora niangamie Wengine wanasema heri nivumilie Kwengine wapi ntapata ajira nambie Na elimu yangu ndo vile mwenzangu na mie Watoto wataishi kwenye yapi mazingira Nikimwambia bwana mkubwa ntaikosa ajira Audio produced by: / majani187 Mixing and Mastering by: / majani187 Video directed by: / majagiking #ferooz #jumanature #bosi