У нас вы можете посмотреть бесплатно WANAWAKE TABORA WANUFAIKA NA SAMIA ARDHI KLINIKI, WAPATA HATI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, wanawake wa Tabora wamejitokeza kushiriki Kliniki ya ufuatiliaji wa Hati za Ardhi inayofanyika katika Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoani humo. Wanawake hao wameipongeza Mamlaka ya Ardhi kwa kuandaa zoezi hilo, wakieleza kuwa limewarahisishia mchakato wa kufuatilia na kupata hati halali za umiliki wa ardhi kwa muda mfupi. Wakizungumza na UFR Machi 4, 2026, baadhi yao wamewahamasisha wanawake wengine wanaomiliki viwanja au mashamba kujitokeza katika Samia Ardhi Kliniki ili waweze kukamilisha taratibu na kupata umiliki rasmi wa ardhi zao. Kwa upande wake, Afisa Usajili msaidizi wa Ofisi ya mkoa wa Tabora (Upande wa Hati), Jenifer Joseph Dominiki, amesema kuwa wakati kliniki hiyo ilipoanza Machi 2, 2026 mwitikio wa wanawake ulikuwa mdogo, lakini kwa sasa idadi imeongezeka na wengi wao wameanza kupatiwa hati zao. Amesema zoezi hilo litahitimishwa rasmi Machi 7, 2026, na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo. Naye Afisa Mipango Miji katika Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Tabora, Suzana Pinini, amesisitiza umuhimu wa kusoma na kuhakiki taarifa zilizopo kwenye hati ili kuthibitisha hati zao zinaendana na eneo husika kabla ya kuzikamilisha. 📻 Sikiliza Uyui FM Radio popote ulipo duniani, bofya kiungo (link) kwenye bio yetu. #2026Fanikisha #tunasambazaunyamwezi #Fanikisha #radioyetusautiyetu