У нас вы можете посмотреть бесплатно Ni nani Aliyetenda Dhambi? | Who Sinned? [18.09.2025] Kuhani James или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Yohane 9:1-12 BHN [1] Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu mmoja, kipofu tangu kuzaliwa. [2] Basi, wanafunzi wakamwuliza, “Mwalimu! Ni nani aliyetenda dhambi: Mtu huyu, ama wazazi wake, hata akazaliwa kipofu?” [3] Yesu akajibu, “Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake. [4] Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi. [5] Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu.” [6] Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni, [7] akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Hapo, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona. [8] Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?” [9] Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi! ” [10] Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?” [11] Naye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: ‘Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.’ Hapo, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.” [12] Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Naye akawajibu, “Mimi sijui!” #somo #live #kuhanijames mzeewayesu