У нас вы можете посмотреть бесплатно AZAM MARINE YAREJESHA SAFARI ZA PEMBA - TANGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, ameishukuru Kampuni ya Azam Marine kwa kurejesha safari za baharini kati ya Pemba na Tanga, akisema hatua hiyo inaleta faraja kubwa kwa wananchi wa mkoa huo. Amesema kurejea kwa safari hizo, zitakazofanyika mara tatu kwa wiki, kutarahisisha usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo, jambo litakalochangia kukuza uchumi wa Tanga na maeneo jirani. Ameongeza kuwa Bandari ya Tanga ni mhimili muhimu wa biashara, hususan kwa usafirishaji wa chakula na bidhaa mbalimbali kwenda Pemba, Zanzibar, Comoro hadi Mombasa. Kwa upande wake, Meneja wa Operesheni wa Azam Marine upande wa Zanzibar, Ali Mohammed Abeid, amesema kuwa kampuni imeamua kuwekeza tena mkoani Tanga baada ya kuongeza boti ya Kilimanjaro Namba Tisa. Amesema kwa kuanzia safari zitakuwa siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili, huku mipango ikiendelea ya kuongeza safari kulingana na mahitaji. Naye Meneja wa Bandari ya Tanga, Salehe Mbega, amesema kurejea kwa Azam Marine kutachochea kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi, akibainisha kuwa biashara kati ya Tanga na Pemba imeongezeka na kiasi cha mizigo kinachosafirishwa ni kikubwa. Wananchi wa Tanga wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kutumia huduma hiyo, huku Azam Marine ikisisitiza kuwa wao si wageni bali wamerejea nyumbani.