У нас вы можете посмотреть бесплатно "Nilikuwa Naitwa Bahili!' Dr Cheni Asimulia A-Z Historia Ya Maisha Yake | SALAMA NA DR CHENI PART 1 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Growing up kwenye mitaa ya Dar es Salaam na TV stations kali wakati huo zilikua na presenters makini na vijana ambao kwa kiasi kikubwa waliifanya tasnia hiyo ipendeze sana. Kuanzia vipindi vya watoto, vya muziki, filamu kutoka nje na tamthilia kutoka nje pia zilikua tamu sana, ukianza kuangalia TV kuanzia jioni hakuna mtu alikua anabanduka mpaka saa nne au tano za usiku, na kama ulikua jobless kama mimi enzi hizo basi ulikua unaunganisha na kuangalia marudio ya vipindi vya muziki ambavyo tayari ulikua ushaviona jioni yake, ila kwasababu ya utamu wake na ku enjoy kile unaona kurudia ilikua easy tu. Sasa likaja wimbi la tamthilia za NDANI, kutoka hapa hapa nyumbani, na nikiwa kama mkazi na mtoto wa Magomeni (Mtaa wa Korongo namba 10 pale kama Downing Street) 🤣 ilikua ma star hawa tunawaona tu kwa mbali na kuwaangalia kwa admiration ya hali ya juu. Cheni, au niseme Dr Cheni naye alikua ni moja ya hao watu, ah, yale ndo yalikua maisha sasa. Yoyote ambaye alikua anapata nafasi ya kuonekana kwenye TV alikua ananyooosha kweli kweli, chochote ambacho anaambiwa ‘acheze’ alikua anakipa uhalisia wa 100%, watu walikua na kiu ya mafanikio sana na jengine kubwa kuliko yote, watu WALIKUA WANAPENDA ambacho WANAFANYA. Na hii simaanishi kumvunjia heshima yoyote yule ambaye anaifanya kazi hiyo leo hii, ila nasemea miaka hiyo ambayo ili uweze kutoboa ilikua inabidi upate ‘upenyo’ ambao nao ukipatikana inabidi uutendee haki sana sana vyenginevyo atatokea mtu huko anakotoka ajipitishe tu kwa miondoko ya ambayo alipita nayo Dr Cheni na kupata nafasi ambayo mpaka leo ndo imefikisha hapo alipo. Again, si kwa ubaya, skuizi unaweza kuwa star wa kwenye social media tu na mambo yako yakakuendea na baada ya mwezi au wiki kadhaa kama huna jipya watu wanakusahau. Dr Cheni anakumbuka kama ilikua jana jinsi ambavyo alipata shavu lake la kwanza la kuwa kwenye mchezo wa kuigiza wa TV, haikua imepangwa na wenye mchezo wao ila yeye alikua amejipanga vizuri tu, alikua amenuia kabisa kwamba vile ndivyo atakavyo fanya ili aonekane na boy alionekana. Kama mtu ambaye tayari alishaanza kushika hela kutokana na kazi zake za udereva, Dr Cheni anakumbuka jinsi ambavyo alianza kuzichanga zile ambazo alikua anazipata kidogo kidogo ili atimize ndoto yake, khadithi yake kwa kiasi flani ilianzia hapo, nami nilitaka kujua hiyo heshima yake na pesa aliitoa wapi? Kutoka kuwa dereva wa daladala mpaka kuwa mmliki wa gari. Huko alifikaje? Na jibu lilikua moja tu, HESHIMA kwa PESA na HESHIMA kwa NDOTO na MALENGO yake. Alifanikiwa sana mwenzetu. Na ndo huyu mpaka leo ambaye bado anaendea kuwepo na upepo kuuhamishia kwenye ku host harusi za watu mbali mbali ambao wengi wao humpa kazi kwasababu tu walishawahi kumuona kwenye TV wakati wanakua, ukiachana na ukweli kwamba yeye ni mmoja kati ya ma MC HODARI kabisa ambao wako sasa kwenye industry hiyo. Akiwa kama Baba mwenye jukumu kubwa la kuiangalia familia yake inavyokua, Dr Cheni anajua kutimiza majukumu na wajibu wake wa kila siku, kupangilia mambo yake ili asiwakwaze wengine ambao wanamtegemea (hasa wale ambao anawafanyia kazi zao za harusi). Kwake yeye kuwa kwenye wakati muafaka ni kila kitu. Na hiyo kwa kiasi kikubwa imesababisha yeye kuwa chaguo la kwanza kwa wengi ambao wanataka sherehe zao zifane. Na je vipi sasa kwenye suala zima la filamu na maigizo? Huko nako kashakimbia? Soko limekaaje? Mipango yake ya baadae je? Yote haya na zaidi yako kwenye lisaa limoja na na dakika 16 ya Podcast hii kama utaskiliza au lisaa limoja la kuangalia naamini litakufungulia mengi. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible &... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz