У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY-THE SCHOOL OF HEALING 19/03/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY-THE SCHOOL OF HEALING 19/03/2026 MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 26 MADA: "KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON) NENO KUU: Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; UJUMBE WA LEO: Sadaka huwa ina tabia ya Kuvuruga fikra na Kutengeneza fikra mpya kwenye UZAO. 1 Wafalme 18 : 37 - 40 37 Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. 38 Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. 39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu. 40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko. Zaburi 49 : 3 3 Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara. 2 Wakorintho 11 : 3 3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka. Ayubu 30 : 2 2 Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini? Watu ambao nguvu zao zimekoma. Mithali 7 : 13-15, 22-26 13 Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, 14 Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; 15 Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. 22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; 23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. 24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. 25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. 26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Mungu anapokupa uzao anakupa na Maelekezo namna ya Kuwatunza na Kuwafikisha kwenye hatma yao Kila anayezaliwa ana Maelekezo yake binafsi. Waamuzi 16 : 17 17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. Kuzimu ikitaka kuvuruga lango la Uzao huwa inavuruga Fikra za wazazi na kupoteza Maelekezo na kusababisha kupoteza uelekeo kwa hilo lango. Watoto wengi wamevurugwa kwa lengo la kukukwamisha lango la Familia na hatma kubwa walioyobeba. Bado unaona watu wako wakiwa na nguvu zao halisi? Je, unapojitizama na kuwatizama wao unaona wakiishi kwenye maisha halisi au wamevurugwa na Vita ya Malezi wamevurugwa na hali za kiroho kutoka kwenye lango la Familia na nguvu zao zimekoma. (Nguvu za kiroho, nguvu za Familia, nguvu za biashara, elimu nk). Nini kimeondoa uwezo kwenye mikono yao, mwanzoni kila walichogusa kilikuwa na matokeo. Nini kimetokea sasa kuna hasara, kuna huzuni, kuna majuto sasa nini kimetokea kwenye hilo lango? Hosea 7 : 9 9 Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari. AGENDA ZA MAOMBI 1. Ombea Nyakati na Majira ya Lango lako la Uzao ambazo zimevurugwa WANAO hamuwezi kufanya vitu kwa wakati na kwa ukubwa na kwa hitimisho. Isaya 33 : 6 6 Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha Bwana ni hazina yake ya akiba. 1 Wafalme 3 : 11 11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 2. Ombea Muda wa UZAO wako ambao umevurugwa na Vita vya lango la Familia (HASA WANAUME). na umewazuia kuwa na hatua mpya kwenye jambo lolote, kuna vita kwenye kila muda wao wa kuinuka, muda wao wa elimu, muda wao wa kuwa na watoto, muda wao wa ndoa, muda wao wa Afya. 2 Wafalme 9 : 8 8 Utafanya hivyo kwa sababu jamaa yote ya Ahabu itaangamia; pia nitamkatilia mbali kila mwanamume wa jamaa ya Ahabu awe mtumwa au mtu huru. Mhubiri: Mwl James Kamera. Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com