У нас вы можете посмотреть бесплатно MAFUNZO YA WHISTLE BLOWING YAONGEZA UWEZO WA WAFANYABIASHARA MIPAKANI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
TCCIA na AGRA Watoa mafunzo ya namna ya kupiga mruzi (Whistle blowing) kwa ajili ya kuboresha biashara za vijana na wanawake za mazao ya chakula mipakani --------------- Kigoma, Novemba 13, 2025 - Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), kwa kushirikiana na Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), inatekeleza mradi unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika biashara za mazao ya chakula kwenye mipaka ya Kibirizi, Mutukula, Sirari na Tunduma. Uzinduzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Kigoma Bw. Obadia E. Kabuga, ambaye amepongeza jitihada za AGRA katika kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, hususan wanawake na vijana. Lengo la Mradi Mradi huu una malengo makuu matatu: 1. Kuongeza ushirikishwaji na mashirika ya u facilitation ya biashara na EAC kutatua NTBs zinazoongeza gharama/muda wa kufanya biashara: 2. Kuimarisha uwezo wa vyama vya sekta binafsi katika masuala ya u facilitation wa biashara, utetezi wa sera, utoaji wa taarifa na matumizi ya nyenzo za u facilitation wa biashara: 3. Kwa kuzingatia umuhimu wa uzoefu katika biashara za mipakani, mradi umejumuisha pia washiriki wachache waliozidi miaka 35 ili kutoa fursa ya kupata uzoefu na ujuzi wa ziada. Uzinduzi wa Booth hizo umeanza kwa mafunzo yanayohusu Whistle blowing ambayo ni pamoja na: Namna ya kukabiliana na vikwazo visivyo vya kikodi (Non-Tariff Barriers) Jinsi ya kuripoti changamoto hizo kwa mamlaka husika kwa kutumia whatsApp Mbinu za kutangaza biashara na kuvutia wateja Ubunifu na uandaaji wa bidhaa zenye ubora kwa ajili ya ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa Mafunzo haya yamepokelewa kwa hamasa kubwa, huku vijana na wanawake wakieleza jinsi yalivyowafungua mawazo na kuwapa ari ya kuendeleza biashara zao. Pia walipata nafasi ya kushiriki changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku za biashara. Sekta Binafsi Kuimarika Kupitia Uwezeshaji TCCIA imesisitiza kuwa uwezeshaji huu ni hatua muhimu katika kujenga kundi la vijana wenye biashara imara, wanaoweza kuongeza uzalishaji na kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa. Kupitia mradi huu, sekta binafsi inatarajiwa kuimarika kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara walioelimika kuhusu masoko, kanuni na taratibu za kikanda.