У нас вы можете посмотреть бесплатно BODI YA KAHAWA KUGAWA MICHE MILIONI 20 YA RUZUKU BURE KWA WAKULIMA NCHINI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Zaidi ya Miche Milioni 20 ya Ruzuku Kugawiwa Bure kwa Wakulima Nchini. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza kwa vitendo mkakati wake wa kuinua sekta ya kahawa kupitia zoezi la ugawaji wa miche ya kahawa ya ruzuku bure kwa wakulima katika kanda mbalimbali za uzalishaji nchini. Kupitia uratibu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, jumla ya miche zaidi ya milioni 20 imeshaanza kugawiwa kwa wakulima katika maeneo yote yanayozalisha zao hilo la kimkakati. Hatua hiyo inalenga kuongeza tija mashambani, kuimarisha ubora wa kahawa ya Tanzania, pamoja na kupanua wigo wa uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Zoezi hilo linaloendelea linaakisi dhamira thabiti ya serikali ya kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima, kuongeza kipato chao na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia zao la kahawa. Jitihada hizi zinaonesha kwa dhahiri namna Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania ilivyojipanga kuleta mapinduzi chanya katika sekta ya kilimo cha kahawa nchini.