У нас вы можете посмотреть бесплатно UJENZI UNAOENDELEA WA KITUO CHA DALADALA NA KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kusini Unguja, Ali Rashid Suluhu, amesema wanaendelea kutekeleza miradi ambayo itakuwa na tija kwa wananchi . Akitembelea miradi ya ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Paje, kituo cha gari za abiria Michamvi na ujenzi wa Soko la biashara katika kijiji cha Kizimkazi, amesema ukamilishwaji wa miradi hiyo itawasaidia wananchi kutofata huduma na mahitaji ya bidhaa na chakula masafa marefu. Nao Wahandisi wa kituo cha gari za abiria michamvi na kiwanja cha kufurahishia watoto Paje, wamesema hatua iliyofikiwa ni ya kuridhisha na inatarajiwa kukamilishwa muda mfupi ujao, ukiwa umekidhi viwango vya ubora unaostahiki . Kwa upande wake mhandisi wa soko la Kizimkazi, Yahya Said Abdallah, kutoka Jeshi la kujenga Uchumi JKU, amesema wako katika hatua ya awali ya ujenzi huo na wanatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa wa miezi mitatu ili kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara. Kituo cha gari za abiria Michamvi na kiwanja cha kufurahishia watoto Paje vinajengwa kwa makusanyo ya fedha za ndani za Halmashauri ya Wilaya kusini na soko la Kizimkazi linajengwa kwa ufadhili wa CRDB bank.