У нас вы можете посмотреть бесплатно MILIONI 10 ZATENGWA KWA ATAKAYE MALIZA FOLENI DAR или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza mkakati kabambe wa kukuza ubunifu wa wahandisi wa ndani kwa kuahidi kuzawadia mawazo ya kibunifu yatakayotatua changamoto zilizopo nchini. Akizungumza na Jumuiya ya Wanafunzi wa Fani za Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo, Ulega amesema mpango huo utahusu wanafunzi wanaosomea taaluma hizo katika vyuo vikuu vilivyopo nchini. Ulega alisema mtazamo wa wizara yake sasa ni kuchochea kada ya wanafunzi wasomi wa uhandisi (mainjinia) ambao watakuwa wanajali zaidi kwenye kutatua kero za taifa lao na si kuwa na maandishi mengi yasiyo na mchango kwenye utatuzi wa changamoto. “Dunia nzima ninyi wahandisi ndiyo mmekuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo. Nchi yetu Ina changamoto nyingi ambazo kwenu zinatakiwa kuwa fursa,” alisema. Katika mkutano huo ulioandaliwa na Ndani ya Uhandisi na Teknolojia (CoET), Ulega alitangaza zawadi ya shilingi milioni 10 itakayogawanywa kwa washindi watatu waliotoa mawazo bora yatakayosaidia jamii zetu. Pia, washindi hao watasaidia kusajiliwa katika Bodi za Kitaaluma, gharama za kufungua kampuni na kupewa mkataba na serikali wa kufanyia kazi wazo lao. “ Fedha ni kichocheo tu lakini ukiwa umesajiliwa, una kampuni na umepewa kazi, utaajiri wengine na ubunifu wako unaweza kutumiwa kwingineko na kuingizia taifa letu fedha za kigeni, “ alisema. Alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan tayari imeahidi kutoa shilingi bilioni 200 kusaidia makundi ya vijana na wanawake na kwamba mpango huu wa wizara yake ni sehemu ya kuongezea kile kilichoanzishwa kwenye uwezeshaji wa makundi hayo. Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba wa UDSM, Ulega pia aliwatia moyo wanafunzi hao kuwa Tanzania ni Taifa linalotoa fursa sawa kwa wote na kwamba mtu mwenye juhudi na maarifa anaweza kuwa yeyote - akitoa mfano wa Yeye mwenyewe ambaye alikuwa mwanafunzi wa UDSM miaka 20 tu iliyopita lakini sasa amepanda hadi kufika alipo.