У нас вы можете посмотреть бесплатно MKUU WA MKOA IRINGA AAGIZA UCHUNGUZI WA HARAKA WA TUKIO LA KUBAKWA NA KUUAWA KWA MTOTO. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Baada ya kuripotiwa tukio la kikatili la kubakwa na kisha kuuawa kwa mtoto wa miaka 13, Naomi Kivamba, mkazi wa Mtaa wa Njia Panda, Kata ya Isakalilo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Leo March 09,2026 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, amefika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kutoa pole na kufuatilia kwa karibu tukio hilo. Akiwa katika eneo la tukio, Mhe. Kheri ameliagiza Jeshi la Polisi kufunga mtaa na kata husika ili kuhakikisha wanawabaini na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na tukio hilo huku akiiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kudhibiti mara moja uuzaji wa pombe za kienyeji majumbani, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu na kuimarisha usalama wa watoto pamoja na wananchi kwa ujumla. Pia Mhe. Kheri amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuimarisha malezi ya watoto, huku akionya dhidi ya uuzaji wa pombe majumbani bila kibali maalumu kutoka kwa mamlaka husika. Aidha Mhe. Kheri, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini vitendo vinavyohatarisha usalama wa watoto na jamii kwa ujumla, ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa na matukio kama hayo yasijirudie tena.