У нас вы можете посмотреть бесплатно POLISI WATOA UFAFANUZI JUU YA MTU ALIYEKUWA ANASAFIRISHA KICHWA CHA MTU KWENYE BEGI👇 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida lingependa kutoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa kwenyemitandao ya kijamii ikimhusu mtu mmoja kutiliwamashaka na wafanyakazi wa Basi namba T794 EHR mali ya kampuni ya Frester lililiokuwa likitoka Kahama kwenda Dar es salaam kuwaanasafirisha kichwa cha mtu(mtoto) baada ya begi lake kutoa harufu kali likiwa ndani ya Gari. Ufafanuzi ni kwamba, Desemba 19,2024 majira ya saa 12.30 jioni huko katika maeneo yamlima Senkenke,Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida,askari wa Jeshi la Polisiwaliokuwa doria katika barabara ya Singida, Nzega walipata taarifa ya taharuki hiyo na kufikaeneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Juma Hamisi Lugendo (30), mkulima na Mkazi waKahama mkoani Shinyanga na kumpeleka kituo kidogo cha Polisi Misigiri kwa ajili ya upekuzi. Aidha, baada ya upekuzi mtuhumiwa huyo alikutwa na vifaa vya uganga wa kienyeji pamoja nadawa za kienyeji zilizochanganywa na utumbo mbichi wa samaki uliopelekea kutoa harufu kalindani ya basi na siyo kichwa cha mtu (mtoto) kama taarifa inavyosambaa kwenye mitandao yakijamii. Hata hivyo, Mtuhumiwa huyo amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kufanyashughuli za uganga wa kienyeji bila kibali. Jeshi la Polis mkoani Singida linatoa onyo kwa wananchi wanaotumia vibaya mitandao yakijamii kwa kutoa taarifa za uongo na kusababisha taharuki katika jamii. Imetolewa na; Amon Daudi Kakwale-SACP. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida. #otvmedia #ngasatv #bosskitana #otvtanzania