У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI MKUU, DK. MWIGULU NCHEMBA, ANATARAJIWA KUANZA ZIARA RASMI YA KIKAZI MKOANI TANGA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya kikazi mkoani Tanga tarehe 13 Februari 2026, kwa lengo la kukagua na kutathmini utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 700. Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wazee wa mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuangalia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na kutoa maelekezo ya serikali kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wananchi. Amesema Waziri Mkuu ataanza ziara yake katika Wilaya ya Handeni, ambapo atakagua jengo la Hospitali ya Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati. Kwa mujibu wa Dkt. Batilda, katika ziara hiyo Waziri Mkuu atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Tanga, ikiwemo miradi ya afya, elimu, miundombinu na sekta nyingine za kijamii na kiuchumi. Ziara hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa wasimamizi wa miradi hiyo, huku Serikali ikiendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu