Π£ Π½Π°Ρ Π²Ρ ΠΌΠΎΠΆΠ΅ΡΠ΅ ΠΏΠΎΡΠΌΠΎΡΡΠ΅ΡΡ Π±Π΅ΡΠΏΠ»Π°ΡΠ½ΠΎ Salama Na MxCarter Ep 6 | LENSMAN Part 2 ΠΈΠ»ΠΈ ΡΠΊΠ°ΡΠ°ΡΡ Π² ΠΌΠ°ΠΊΡΠΈΠΌΠ°Π»ΡΠ½ΠΎΠΌ Π΄ΠΎΡΡΡΠΏΠ½ΠΎΠΌ ΠΊΠ°ΡΠ΅ΡΡΠ²Π΅, Π²ΠΈΠ΄Π΅ΠΎ ΠΊΠΎΡΠΎΡΠΎΠ΅ Π±ΡΠ»ΠΎ Π·Π°Π³ΡΡΠΆΠ΅Π½ΠΎ Π½Π° ΡΡΡΠ±. ΠΠ»Ρ Π·Π°Π³ΡΡΠ·ΠΊΠΈ Π²ΡΠ±Π΅ΡΠΈΡΠ΅ Π²Π°ΡΠΈΠ°Π½Ρ ΠΈΠ· ΡΠΎΡΠΌΡ Π½ΠΈΠΆΠ΅:
ΠΡΠ»ΠΈ ΠΊΠ½ΠΎΠΏΠΊΠΈ ΡΠΊΠ°ΡΠΈΠ²Π°Π½ΠΈΡ Π½Π΅
Π·Π°Π³ΡΡΠ·ΠΈΠ»ΠΈΡΡ
ΠΠΠΠΠΠ’Π ΠΠΠΠ‘Π¬ ΠΈΠ»ΠΈ ΠΎΠ±Π½ΠΎΠ²ΠΈΡΠ΅ ΡΡΡΠ°Π½ΠΈΡΡ
ΠΡΠ»ΠΈ Π²ΠΎΠ·Π½ΠΈΠΊΠ°ΡΡ ΠΏΡΠΎΠ±Π»Π΅ΠΌΡ ΡΠΎ ΡΠΊΠ°ΡΠΈΠ²Π°Π½ΠΈΠ΅ΠΌ Π²ΠΈΠ΄Π΅ΠΎ, ΠΏΠΎΠΆΠ°Π»ΡΠΉΡΡΠ° Π½Π°ΠΏΠΈΡΠΈΡΠ΅ Π² ΠΏΠΎΠ΄Π΄Π΅ΡΠΆΠΊΡ ΠΏΠΎ Π°Π΄ΡΠ΅ΡΡ Π²Π½ΠΈΠ·Ρ
ΡΡΡΠ°Π½ΠΈΡΡ.
Π‘ΠΏΠ°ΡΠΈΠ±ΠΎ Π·Π° ΠΈΡΠΏΠΎΠ»ΡΠ·ΠΎΠ²Π°Π½ΠΈΠ΅ ΡΠ΅ΡΠ²ΠΈΡΠ° ClipSaver.ru
#YAHStoneTown #SalamaNa #MxCarter Listen our Podcast on Boomplay Link https://boomplay.lnk.to/SalamaNaβ¬ βͺSpotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cmβ¬ βͺApplePodcasts Link https://apple.co/2Ou1bruβ¬ βͺYouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa LENSMAN Touch yake katika mambo mengi ndo ambayo inamfanya awe tofauti sana na vijana wengine walokuja mjini nae kwa wakati mmoja, uzuri ni kwamba nilikuwepo wakati mabegi (kama yalikuwepo) hata hayajatua uzuri chini ndo hapo nilikutana na Mashala, aka Michael Sylvester βCarterβ Mlingwa. Kwanza ilikua kujuana kwa kwenye mitandao tu na hiyo ni khadithi ya siku nyengine. Kwa wanao nifahamu mimi wanajua kama ni ngumu haswa kumuingiza mtu katika maisha yangu, awe karibu yangu, ajue undani wangu ndo maana nina watu wengi ninaofahamiana nao ila wanaonijua ni wachache. Michael ni mmoja ya watu wanaonijua mimi, na naweza kusema nami namjua yeye. Makutano yetu ya kwanza yalikua kwenye kibaraza cha MJ Records pale nje kwa Marco Chali, nakumbuka mpaka alikua kavaa nini, jeans moja kichupa ivi na fulana ya rangi ya udhurungi, mkononi alikua bracelet ya kimasai zile zinazofunika nusu mkono (mawindo ya wazungu yalikua yanahusiana na muonekano π€£), chini alikua na raba tu simple na begi lake la mgongoni. Wembamba wake ulikua unamfanya aonekane mrefu na rangi wake ulikua utani na mfano kwa kila mtu tutakayemuona ana rangi inayoshabihana na yake. Michael alikua na yake ya kufanikiwa moyoni toka siku ya kwanza ila kikubwa zaidi ni roho yake nzuri na kutaka kila mtu anayetaka msaada kwake afanikiwe na hata wale ambao hawajui alikua akiwatafuta aongee nao ili awaelekeze jinsi ya kufanya baadhi ya vitu ili wajiongezee kipato, haswa wanamuziki. Nakumbuka aliponunua gari yake ya kwanza, alikua ananiachia mimi niendelee nalo na mitkasi yangu kisha yeye anapanda bajaji, si mara moja wala mbili, wala tatu, roho ya aina hii bila ya shaka ndo imemfanya awe anazidi kubarikiwa. Kwa kipindi kisichozidi miaka kumi jamaa yangu huyo amepiga hatua kubwa katika maisha pengine kuliko kijana mwengine yoyote ambae mimi nilimuona toka mwanzo akiwa amefika βtownβ. Kukaa nae kwenye meza halikua jambo la mjadala maana safari yake ya kutoka kushika camera mpaka kuwa kiongozi wa kampuni yake mwenyewe na kuwaajiri vijana wenzake na kuwa partner wangu kwenye biashara hii unayoitizamana nadhani anafaulu kwa alama za juu kabisa. Hapa tunakugusia maisha yeke ya utotoni, shughuli za Marehemu Mzee wake, kukua katika familia yenye watoto wengi, mahusiano yake na watu wa mjini na jinsi ambayo ameweza kuepuka kifo mara mbili kwa ajali ambazo moja alitakiwa kabisa awemo na pengine saa hii tungekua tunasema mengine. Ila kubwa kuliko ni kusoma njia alizopita ili nawe uweze kujifunza jambo. Tafadhali enjoy. Love, Salama. Follow: Twitter: Β Β /Β yahstonetownΒ Β Instagram: Β Β /Β yahstonetownΒ Β Facebook: Β Β /Β yahstonetownΒ Β