У нас вы можете посмотреть бесплатно SDA YATOA MAFUNZO YA SHERIA YA MPIRA WA PETE ( NETBALL) NEWALA MJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Shirika lisilo la kiserikali la Sports Development Aid (SDA) March 23, 2024 limeendesha mafunzo ya mchezo wa mpira wa Pete (Netball) kwa wanafunzi, walimu, na viongozi wa serikali kutoka katika kata tano za Halmashauri ya mji Newala zilizopo Kwenye Mradi ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuzitambua Sheria za mchezo huo ili wajiamini na kupelekea kufanya vizuri kwenye masomo yao. Akizungumza katika mafunzo hayo afisa utamaduni na michezo Halmashauri ya Mji Newala Ndugu Faraji Hamisi, amewapongeza SDA kwa kuona umuhihu wa kufundisha mchezo huo kwani itawasaidia kufanya vizuri katika mashindano ya umiseta na umitashuta yanayotarajia kuanza hivi karibuni. Aidha Ndugu Faraji amewasihi wanafunzi kushiriki michezo kikamilifu ili iwaletee maendeleo kwani kwa sasa serikali imewekeza katika michezo. Kwaupande wake kaimu mtendaji kata ya Maumbika Bi Neemaeli Amani amewasisitiza waalimu kwenda kusimamia Sheria zilizofundishwa ili wanafunzi wacheze kikamilifu mchezo huo tofauti na sasa ambapo wanafanya makosa mengi tofauti na taratibu zilizopo Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake walioshiriki mafunzo hayo Faima Hamnza mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka sekondari ya kutwa Mtumachi ametoa shukrani kwa shirika la SDA kwa kuwapatia mafunzo kwani awali walikuwa wakifanya makosa mengi wakati wakicheza mchezo huo Nae mwezeshaji kutoka Shirika la SDA Newala Ndugu Denis Malima amewasihi walimu kuwapa wanafunzi nafasi ya kushiriki michezo hasa watoto wakike kwani inawasaidia muwaepusha kukutana na vitu vya tofauti vinavyoweza kukatisha masomo yao