У нас вы можете посмотреть бесплатно Mfahamu Prof. Mahalu, Balozi aliyempandisha Rais Mkapa kizimbani kutoa ushahidi или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tanzania imepoteza mmoja wa wasomi na wanadiplomasia wake mahiri, Profesa Costa Ricky Mahalu,aliyelitumikia vyema Taifa na kuacha alama katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya elimu ya juu na sheria. Ukurasa wa maisha yake ulifungwa rasmi machi 9, 2026 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam baada ya kuishi kwa takribani miongo saba, miaka saba na miezi nane. Licha ya mchango wake uliotukuka katika Taifa Mwaka 2007, Profesa Mahalu alikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin. Pamoja na kuwa kesi hiyo iliisha miaka mingi iliyopita, kumbukumbu yake imebakia kwenye vichwa vya wengi na kuacha rekodi ya pekee katika historia ya mahakama Tanzania. Upekee wa kesi hiyo ulitokana na aina ya mashahidi waliotajwa husussan upande wa utetezi akiwemo rafiki yake wa karibu Hayati Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu nchini Tanzania.