У нас вы можете посмотреть бесплатно MKESHA WA MAOMBI KKKT-DKMs TAREHE: 20/03/2026. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Made with Restream. Livestream on 30+ platforms at once via https://restream.io Unatazama mubashara Mkesha wa maombi kutoka KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto. KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, chini ya uongozi wa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, imeendelea na utaratibu wake wa kila mwaka wa kufanya Maombi ya Mwezi Mzima. Kwa mwaka huu wa 2026, maombi haya yalianza rasmi tarehe 22.02.2026 na yanahitimishwa tarehe 20.03.2026. Ibada ya uzinduzi wa Mwezi wa Maombi ilifanyika tarehe 22.02.2026 katika Usharika wa Bungu. Kilele cha maombi haya kidayosisi kinafanyika katika Jimbo la Kusini, Usharika wa Bumbuli, kwa ibada ya mkesha leo Ijumaa tarehe 20.03.2026. Katika siku 10 za mwisho za mwezi huu wa maombi, yaani kuanzia tarehe 11.03.2026 hadi 20.03.2026, kumekuwa na maombi ya mnyororo kwa masaa 24 kila siku. Wanadayosisi pamoja na vikundi vyote vya maombi wamejitokeza kikamilifu kushiriki katika kumwomba Mungu. Katika kipindi hiki, mambo mbalimbali yamewekwa mbele za Mungu, yakiwemo: Kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake uliotuwezesha kuingia salama katika mwaka wa 2026. Tunaamini Mungu ana kusudi na kila mmoja wetu katika mwaka huu. Kumshukuru Mungu kwa kupunguza deni la Dayosisi, ambapo waumini wengi wamefanikiwa kukamilisha michango yao. Tunamshukuru Mungu kwa kuwezesha baadhi ya sharika kumaliza kabisa sehemu yao ya deni. Kwa ujumla, deni limepungua kutoka shilingi bilioni 7.6 mwaka 2021 hadi kufikia bilioni 2.8 mwezi Januari 2026. Kumuomba Mungu atupe nguvu, afya na mafanikio, ili kwa umoja wetu tuweze kumaliza deni lililobaki. Mungu azibariki kazi zetu zote ili tuweze kumtumikia kwa ufanisi. Kuwaombea vijana wa Dayosisi, hasa katika mwaka wao wa Vijana DKMS, ili watimize malengo yao ya kuwa mashahidi wema wa Yesu Kristo. Vijana waendelee kusimama imara kupinga upotoshaji wowote unaoweza kuharibu maadili ya Kikristo. Kumuomba Mungu atuimarishe katika umoja wa kweli, ili tushikamane katika kutekeleza majukumu yetu ya kiroho na kijamii. Mungu awavutie kwake wale wote wanaosababisha chuki na migawanyiko. Kuliombea Taifa letu la Tanzania, ili liendelee kuwa na amani ya kweli. Tumuombe Mungu awajalie viongozi wetu hekima na uwezo wa kuongoza kwa haki na uadilifu. Kuzibariki familia zetu, ili ziendelee kuwa na upendo, mshikamano na ushirikiano, kwani familia ndiyo msingi wa Kanisa la Mungu hapa duniani. Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii INSTAGRAM - / elctned FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV WEBSITE: www.elctned.org