У нас вы можете посмотреть бесплатно Funga mwaka na Chief Waitala или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ndugu mtazamaji na msikilizaji wa Uchochoro TV, karibu sana. Mimi ni yule yule, mpambanaji wa urithi wa Afrika, Maswi Magige, mwandaaji na msomaji wako wa makala haya. Leo tunawaletea tukio maalum lililofanyika nyumbani kwa Chief na Mbunge wa Tarime Vijijini, katika Kijiji cha Kangaliani, Jimbo la Tarime Vijijini. Tukio hili liliandaliwa na Mheshimiwa Mbunge wa Tarime Vijijini na Chief wa Wailege, Mwita Mwikwabe Waitala, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo aliandaa sherehe kubwa ya kijamii aliyoiita: “Funga Mwaka na Chief Waitala.” Sherehe hii ilikuwa na lengo la kuwaleta pamoja wananchi, viongozi, wazee wa kimila, vijana pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii, kwa ajili ya mshikamano, furaha, na kuendeleza mila na desturi zetu za asili. Katika sherehe hizi, Hata hivyo sherehe hizo zilifanikiwa sana, watu kutoka maeneo mbalimbali walifika, wakiwemo viongozi Chama na serikali ngazi ya mkoa, wilaya, kata na vijiji, na hata vitongoji. Mheshimiwa Mbunge alialika vikundi mbalimbali vya muziki wa asili, vikiwemo vikundi vinavyoenzi utamaduni na historia ya jamii ya Wailege pamoja na makabila jirani. Miongoni mwa vikundi hivyo ni Kikundi cha Nyaghetarya, ambacho kilitoa burudani ya kipekee ya muziki wa asili, iliyovutia na kugusa hisia za wengi. Kilichovutia zaidi katika tukio hili ni namna ambavyo Mheshimiwa Mbunge Mwita Mwikwabe Waitala mwenyewe alishiriki moja kwa moja, akiungana na kikundi cha Nyaghetarya, akicheza, kuimba, na kuonesha kwa vitendo mapenzi yake ya dhati kwa utamaduni wetu. Kama shuhuda wa kweli uchochoro tv Hapa tunawasilisha taswira halisi ya ushiriki huo, tukio lililodhihirisha wazi kuwa uongozi bora haujitengi na watu wake, bali huishi nao, husherehekea nao, na kuheshimu mizizi ya jamii anayowakilisha. Endelea kutazama video hii kwa makini, ujionee mwenyewe mshikamano, furaha, na uzalendo wa kitamaduni uliodhihirishwa katika sherehe ya Funga Mwaka na Chief Waitala. Asanteni sana kwa kutazama