У нас вы можете посмотреть бесплатно ERB YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA UJENZI - IRINGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imefanya ukaguzi wa miradi ya kihandisi inayotekelezwa katika Mkoa wa Iringa kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa sheria, kanuni na viwango vya taaluma ya uhandisi. Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo) – Kilolo, barabara ya Iringa Bypass pamoja na barabara ya Iringa – Msembe yenye urefu wa kilometa 104. Ukaguzi huo uliongozwa na Mkuu wa Idara ya Udhibiti ERB, Mhandisi Erick Nestory, ambaye ameridhishwa na kiwango cha utekelezaji na uzingatiaji wa sheria katika miradi hiyo. Katika mradi wa Iringa – Msembe, Mhandisi wa Madaraja wa mradi huo, Mhandisi Marseli Timo, alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 104 inaanzia Iringa Mjini hadi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha National Park. Alieleza kuwa mradi huo ni wa miaka miwili na ulianza kutekelezwa Februari mwaka jana na kwa sasa umefikia asilimia 29 ya utekelezaji, ambapo utakapokamilika utakuwa na madaraja makubwa matatu yatakayorahisisha usafiri na kuchochea shughuli za utalii. Aidha, ERB ilikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo) – Kilolo yenye urefu wa kilometa 33.61 ambapo hadi sasa umefikia asilimia 96 ya utekelezaji Kwa upande wa mradi wa barabara ya Iringa Bypass, Mhandisi wa Miradi kutoka ofisi ya TANROADS Mkoa wa Iringa, Mhandisi Salum Mwinuka, alisema barabara hiyo ina urefu wa kilometa 7.3 kutoka Ihumbilu hadi kuunganisha na barabara ya Iringa – Dodoma, na kwa sasa mradi umefikia asilimia 35 ya utekelezaji wake. Akihitimisha ukaguzi huo, Mhandisi Erick Nestory alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za uhandisi ikiwemo usajili wa miradi na wahandisi wanaosimamia miradi hiyo. Pia aliwataka wahandisi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kufika katika ofisi za TANROADS Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuhuisha leseni zao katika kambi maalum ya siku tano iliyoandaliwa na ERB jijini hapo.