У нас вы можете посмотреть бесплатно Sanguine Personality / Jitambue Haiba Yako Ili Ufikie Maono Yako Kirahisi / Jane Kimaro или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 11/ 11/ 2024 MAFUNGO YA SIKU 40 - SIKU YA 8 UJUMBE WA LEO: ''WEKEZA KWENYE UWEZO WAKO" "INVEST IN YOUR CAPABILITY" NENO KUU : Waamuzi 6 : 14 ENENDA KA UWEZO WAKO HUU UJUMBE WA LEO : JITAMBUE HAIBA YAKO ILI UFIKIE MAONO YAKO KIRAHISI MAMBO MAKUU YA KUJIFUNZA . KUJUA MAARIFA ILI KUSAIDIKA . AINA KUU NNE ZA HAIBA (PERSONALITY) . FAIDA YA KUJUA HAIBA YAKO. HOSEA 4:6a Watu wangu wnaangamizwa kwa kukosa maarifa; Maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida au kupata kitu kwa kutumia elimu au ujuzi fulani, ujuzi huo unaweza kuwa wa kuzaliwa au kuupata kwa kusoma , kusikia au kutenda. mithali12:1 Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa. Pia ni ufahamu na uelewa kama ulivyofundishwa au maongozi ya Roho mtakatifu HAIBA -PERSONALITY Haiba au personality ni muonekano wa mtu kwa ujumla, kimavazi na jinsi unavyoonekana watu wakikutazama, Haiba pia ni hali ya kiundani zaidi na pana sana inayomuelezea mtu fulani, inajumuisha sifa za utu, mifumo dhabiti ya mawazo, hisia na matendo yanayomtofautisha mtu na mtu mwingine. Wanasaikologia waliweza kuielezea haiba miaka zaidi ya elfu mbili huko nyuma. Kuna aina kuu nne za haiba (personality) 1. CHOLERIC 2. SANGUINE 3.MELANCHOLIC 4 . PHLEGMATIC SANGUINE PERSONALITY Inajulikana kama "Haiba ya Kijivu" au "Mtu mwenye haiba ya furaha". Hawa ni watu wanaojulikana kwa kuwa wachangamfu, wana marafiki wengi Mithali 18:24 , na wenye furaha Mithali 15:13. Mara nyingi, wana msisimko wa maisha, wanapenda kushirikiana na wengine, na wana tabia za kijamii na kuongea sana kwa sauti ya juu. Watu wenye haiba hii huwa na nguvu nyingi za mvuto, wanavutia kwa urahisi, na wanapenda kujaribu mambo mapya, ni wachangamfu sana Hata hivyo, wanaweza pia kuwa wapuuzi kwa urahisi Mithali 15:12 au wasiojali sana mipango ya muda mrefu, kwani wanapenda kuishi kwa wakati uliopo na kujifurahisha.Ni wacheshi wanamatumaini,Hawawezi kutunza jambo(fridge haligandishi) Mithali 10:19, hawana aibu,hawana utulivu. SANGUINE Anaongozwa na hisia za nje na anamsisimko sana, hivyo kuwa makini na ahadi za sanguine mara nyingi hazina uhalisia.They are so emotional. Hawana mpangilio wa vitu hivyo msaidie katika kupangilia mambo yake. Sio wazuri kwenye ufuatiliaji wa mambo hivyo kama anasimamia jaambo ni vizuri kujua kafikia wapi japo anaweza kukukdanganya kuwa makini unapomfuatilia sanguine. Wanapuuzia mambo ambayo saa nyingine wanaweza kupoteza fursa , kwa sababu hawaweki kipaumbele kwenye mambo muhimu lolote linalokuja mbele yake ni muhimu kwake kwa wakati huo. Hawatafakari mambo kwa kina, hivyo hufanya maamuzi ya haraka bila kutafakari. Msaidie kupangilia mambo yake hata kwa kupanga ratiba yake ya siku, mwezi , mwaka. Ni wepesi kuvutwa na vitu visivyo muhimu kama michezo , story safari zisizopangiliwa. Hawana muda wa kuchunguza mambo. Wanashida kwenye kipaumbele nini cha kufanya kwanza. Hawana uwezo wa kutunza siri, hivyo kuwa makini unapomshirikisha mambo yako hasa ya siri. Hawamanishi kile wanachosema , kwa hiyo usiamini kwa asilimia 100 kile wanachosema Hawapendi kukosa furaha hivyo huitafuta kwa gharama yoyote kama club, kwaya kanisani mpira au kusafiri. Mhubiri: Mwl. Jane Kimaro Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053