У нас вы можете посмотреть бесплатно BANDARI YA DAR YAWEKA REKODI KWA KUHUDUMIA MELI KUBWA ZAIDI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Dar es Salaam. Malengo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa kitovu cha kuhudumia shehena ya mizigo kwa nchi jirani yameanza kuonekana, baada ya bandari hiyo kuanza kupokea meli kubwa zenye urefu wa hadi mita 300. Mafanikio hayo yametokana na maboresho makubwa yaliyotekelezwa na Serikali kupitia Mradi wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP) chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa mara ya kwanza, bandari hiyo imehudumia meli kubwa aina ya Post Panamax, Mv. MYNY, yenye urefu wa mita 300 na uwezo wa kubeba tani 75,201 ikiwa na makasha 6,840. Mkurugenzi wa Marine na Shughuli za Kibandari, Kapteni Abdallah Mwingamno akizungumza leo Ijumaa, Septemba 5, 2025 amesema tukio hilo ni uthibitisho wa uwezo mpya wa bandari hiyo kuhudumia meli kubwa za kisasa. Amesema mbali na maboresho ya gati, Serikali pia imewekeza kwenye mitambo ya kisasa ikiwemo Ship to Shore Gantry Cranes (STS) na Rubber Tyred Gantry Cranes (RTG), hatua inayopunguza muda wa meli kukaa bandarini. Kupitia DMGP, gati namba 1–7 zimeimarishwa kwa kuongeza kina hadi mita 14.5, eneo la kugeuzia meli limefikia mita 15 na lango la kuingilia limepanuliwa. Mradi huo wenye thamani ya Sh1.118 trilioni, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na mapato ya ndani ya TPA, unaweka Tanzania kwenye nafasi ya ushindani mkubwa Afrika Mashariki na Kati.