У нас вы можете посмотреть бесплатно HII HAPA TU-160M, NDEGE YA RUSSIA INAYOOGOPWA NA TRUMP, MATAIFA YA ULAYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Inaitwa Tupolev ama Tu-160M, pia hujulikana kama “White Swan” iliyopewa jina la Blackjack na Jumuiya ya Kujilinda na NATO. Hii ni ndege ya kivita ya kasi ya juu yenye mabawa yanayoweza kubadilishwa, iliyotengenezwa na Russia na sasa inatumiwa na Jeshi la Anga la Russia. Ndege hii ni kilele cha teknolojia ya ndege za kivita za enzi ya Kisovyeti na bado ni sehemu muhimu ya kikosi cha ndege za kimkakati za Russia. Makala hii inayoletwa kwako nami Mgongo Kaitira inachunguza historia, muundo, uwezo, na hali ya sasa ya ndege hii tishio inayowanyima usingizi Marekani na mataifa ya Ulaya aina ya Tu-160M. Tu-160: Ndege la Russia inayofanana na ndege ya kivita ya Marekani aina ya B-1 Lancer Historia ya ndege hii tishio ya Russia inaturudisha nyuma ambapo maendeleo ya Tu-160 yalianza miaka ya 1970 kama jibu la kisasi dhidi ya ndege ya kivita ya Marekani aina ya B-1 Lancer. Umoja wa Kisovieti ulitaka ndege ambayo ingeweza kupenya ndani kabisa ya eneo la adui kwa kasi na urefu mkubwa, ikibeba silaha za kawaida na za nyuklia. Mashindano ya kubuni ndege hii yalizinduliwa mwaka 1972, na Shirika la kubuni ndege za kijeshi la Tupolev ambalo ndiyo lilishinda kandarasi hiyo. Tu-160 ilifanya safari yake ya kwanza Desemba 18, 1981 na kuanza kutumika rasmi Aprili 1987. Ilikuwa ndege ya mwisho ya kimkakati kubuniwa kwa Jeshi la Anga la Kisovyeti kabla ya kuvunjika kwa Muungano huo. Uzalishaji uliendelea hadi 1992, na jumla ya ndege 36 zilitengenezwa. Baada ya kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti, ndege hizo ziligawanywa katika mataifa ya Russia na Ukraine, ambapo baadaye Russia ilichukua idadi kubwa ya ndege zilizokuwa nchini Ukraine. MANENO MAWILI: BOMU LA KASI SANA Tu-160M ndiyo ndege kubwa na nzito zaidi ya kivita duniani, na pia ndiyo ndege yenye kasi zaidi inayotumika kwa sasa. Ndege hii ina mabawa yanayoweza kubadilishwa kulingana na hali ya hewa na kasi, kwa ajili ya utendaji bora ukiwemo wa kutengeneza mbwembwe ikiwa angani. Ndege hii inabeba wafanyakazi wanne: rubani, msaidizi wa rubani, mnajimu wa safari, na ofisa wa vita vya kielektroniki. Sifa nyingine ni kwamba ina urefu wa futi 177 na inchi 6, upana wa mabawa wa futi 182 na inchi 9 yakiwa yamepanuliwa kikamilifu, na futi 116 na inchi 10 yakiwa yamekunjwa. Pia ina urefu wa futi 42 na inchi 12, na uzani wa juu wa kuruka ni paundi 606,271. Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa mashirika ya habari.