У нас вы можете посмотреть бесплатно ATHARI ZA KIMBUNGA HIDAYA MAFIA WANANCHI WAKOSA MAKAZI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Siku chachu baada ya malamaka ya hali ya hewa Tanzania TMA kutangaza taarifa ya kuwepo viashiria vya kutokea kwa kimbunga Hidaya kuanzia tarehe tatu hadi tarehe sita mwezi huu, wananchi wa wilaya ya Mafia mkoani Pwani wamekumbwa na kimbunga hicho kilichosababisha uharibifu mkubwa wa nyumba za mali zao ikiwemo kuharibu vibaya mindombinu ya barabara na umeme katika maeneo mengi wilayani humo. Wananchi waliofikwa na Kimbunga hicho kutoka katika kata nane na tarafa mbili za wilaya Mafia wameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la kipekee ili wapatiwe malazi, chakula na mavazi ili kuwawezesha kujihifadhi kwa kipindi hiki cha mpito kwani hivi sasa wanalazimika kulala kwa ndugu baada mapaa ya nyumba zao kuezuliwa vibaya kufuatia kimbunga hicho kilichoharibu miundombinu ya umeme na barabara. Kufuatia taharuki hiyo Mkuu wa wilaya Mafia MH. Aziza Mangosongo ametembelea maeneo yaliyokumbwa na kadhia hiyo ili kuwajulia hali wananchi waliokumbwa na Kimbunga kilichoharibu makazi pamoja na mali zao huku akiwataka wale wanaofanya shughuli zao baharini kuhakikisha wanatii maagizo yanayotolewa viongozi ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.