У нас вы можете посмотреть бесплатно SKANKA YAKUTWA NDANI YA LORI LA MATUNDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imefanikiwa kukamata tani 9.93 za dawa za kulevya, chupa 1,795 za dawa tiba zenye asili ya kulevya, na kuteketeza ekari 87.5 za mashamba ya bangi. Katika operesheni hizo nchi nzima, watuhumiwa 151 walikamatwa pamoja na magari sita na pikipiki 29 vilivyokuwa vikitumika kufanikisha uhalifu huo, huku bangi aina ya skanka ikionekana kukamatwa kwa wingi. Jijini Dar es Salaam, mtuhumiwa mmoja alikamatwa eneo la Kibamba akiwa na kilogramu 81.883 za skanka zilizofichwa kwenye lori la matunda lenye usajili wa Afrika Kusini, wakati eneo la Chanika watuhumiwa wawili walinaswa na kilogramu 488.64 za dawa hizo. Jitihada hizo za mamlaka zimeendelea kuwabaini wasafirishaji wanaotumia mbinu mbalimbali za kificho ili kupitisha dawa hizo haramu sokoni. Aidha, ukaguzi uliofanywa kwenye mabasi ya abiria jijini Mbeya uliwawezesha maofisa kuwakamata watuhumiwa sita kwa nyakati tofauti, akiwemo raia wa Malawi, wakisafirisha shehena ya skanka. Watuhumiwa hao walikutwa na kiasi tofauti cha dawa hizo, kuanzia kilogramu 4.62 hadi 46.46, hali inayoashiria kuimarika kwa udhibiti katika njia kuu za usafiri nchini. Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania #Follow @itvtz @radioonetanzania @capitaldigitaltanzania. Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3 Twitter : https://bit.ly/2XG7aii Instagram : https://bit.ly/34KItmg