У нас вы можете посмотреть бесплатно CCM TABORA YATANGAZA HATUA ZA NDANI KUTAFUTA WAGOMBEA WA3 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
TABORA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora kimeeleza kuvutiwa na idadi kubwa ya wanachama ambao wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, hali inayotajwa kuwa ni kielelezo cha imani ya wananchi kwa chama hicho pamoja na kuimarika kwa demokrasia ya ndani ya chama. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tabora , Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM mkoa wa Tabora, Bw. Iddy Moshi Mambo, amesema jumla ya wanachama 152 wamechukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, huku wanawake 21 wakijitokeza kuwania ubunge kupitia viti maalum vya UWT, mmoja kupitia Wazazi, na wawili kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM). Kwa upande wa udiwani, wanachama 1,225 wamechukua fomu, kati yao wanaume 1,086 na wanawake 139, ambapo hadi kufikia mwisho wa mchakato huo wanaume 933 na wanawake 125 wamesharejesha fomu, idadi inayofikisha jumla ya 1,220 ambao wamerejesha fomu kwa nafasi hiyo. Aidha, madiwani wa viti maalum waliochukua fomu kutoka wilaya zote saba za mkoa huo wamefikia 243. Bw. Mambo amesema, licha ya ongezeko hilo kubwa, chama kinatarajia kuwa na kazi ngumu katika mchujo wa kuwachuja wagombea, kwani takribani wote waliorejesha fomu wanakidhi vigezo vya msingi ambapo Kwa mujibu wa takwimu, kati ya wanachama 132 waliogombea ubunge, asilimia 86 wana elimu ya chuo, 11 wana elimu ya sekondari, na 10 sawa na asilimia 7 wana elimu ya darasa la saba. Mh Iddy Mambo amewataka wanachama wote waliojitokeza kuwania nafasi hizo kuendelea kuwa watulivu, watiifu, na kuepuka kuingia kwenye malumbano, kauli za kuchafuana, au vitendo vinavyoweza kuharibu taswira ya chama wakati mchakato ukiendelea. Mchakato wa mchujo umeanza rasmi leo ngazi ya kata, na unatarajiwa kukamilika Julai 20, 2025 kwa ngazi ya taifa, ambapo wagombea wenye sifa na waliokubalika kwa wananchi ndio watakaopitishwa kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo: / spotileo-176. . HabariLeo: / habarileo DailyNews: / dailynewstz INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09