У нас вы можете посмотреть бесплатно Utanuzi Uwanja wa NDEGE Pemba waanza или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WUMU IMEANZA ZOEZI LA UTAMBUZI NA UHAKIKI WA UTANUZI WA ENEO LA UWANJA WA NDEGE PEMBA Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Matar Zahoro Masoud amewataka wananchi ambao maeneo yao yanatarajiwa kutumiwa kwa ajili zoezi la utanuzi wa Kiwanja cha ndege cha Pemba kuwa wavumilivu wakati Serikali imeanza kazi ya utambuzi wa maeneo kupitia kamati iliuondwa na Waizara ya Ujenzi, Mawasiliano na uchukuzi. Mhe. Matar ameelez hayo wakati alipofanya ziara maalum ya kukagua zoezi linaloendelwa katika shehia ya Mfikiwa na Mvumoni Mkoa wa Kusini Pemba. Aidha, Mhe. Matar amezipongeza kamati maalum zilizoundwa na Wizara kwa kasi kubwa wanayoendeIea nayo katika kufanya uhakiki na utambuzi wa zoezi hilo. Kwa upande wake Afisa mdhamin wa Wizara ya Ujenz, Mawasiliano na Uchukuzi ndugu Ibrahim Saleh Juma amemuhakikishia Mhe. Mkuu wa Mkoa wa kusini kuwa, zoezi hilo litakamilika ndani ya muda mfupi ili kuruhusu zoezi jengine la ufanyaji wa tathmini kwa mali za wananchi hatimae kulipwa fidia wanazostahiki. Pia, Afisa mdhamin Ibrahim amewaomba wananchi kutoendelea na harakati zozote za ujenzi kwa mpaka pale zoezi hili litakapokamilika ili Serikali uweze kulitambua eneo litakolotumika. Kamati hizo zilizoundwa tayari wameshafanya utambuzi wa nyumba pamoja na maeneo sambamba na kuanza zoezi la uwekaji wa alama katika eneo litakalotumika. Imetolewa na Kitengo cha Habari (WUMU). Febuari 07, 2023.