У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/02/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/02/2026 MAFUNGO YA KWARESMA 2026. SIKU YA 2 UJUMBE WA LEO: KUTOKA MSIMU MPAKA KUSUDI ( MSAADA WA MUNGU UNAPOSHAMBULIWA NA MSIMU KWENYE KUSUDI ) Ruthu 1 : 11 - 22 11 Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? 12 Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; 13 je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu. 14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye. 15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako. 16 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami. 18 Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye. 19 Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20 Akawaambia, Msiniite Naomia, niiteni Marab, kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. 21 Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? 22 Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri. MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU SHAMBULIZI LA MSIMU KWENYE KUSUDI. ➡️Kila shambulizi lina kusudi la kiroho Hujaribu imani, kuimarisha subira, au kuandaa mtu kwa baraka (kusudi). ➡️ Shambulizi la misimu linaonesha mzunguko wa maisha dhoruba → uvumilivu → (Kusudi) mafanikio. ➡️Kushikilia Kusudi la Mungu wakati wa Shambulizi la msimu (dhoruba) hutoa thawabu kubwa mfano Naomi. ( Mama wa uzao wa kifalme) MISIMU UNAPOSHAMBULIWA KUSUDI NI LAZIMA KUWEPO. 1️. KUWEPO DHIKI FULANI NJAA, MAUTI AU UTASA. 2️. MAAMUZI FULANI YATALAZIMIKA KULINGANA NA JINSI ULIVYOFIKIWA NA SHAMBULIZI. 3. MATOKEO (MABADILIKO HUJA) CHANYA AU HASI HUTOKEA. MASHAMBULIZI YA MSIMU KWENYE KUSUDI LA NAOMI, ORPA NA RUTHU ➡️ Naomi Shambulizi la Mauti / Uchungu Mkubwa: Kifo cha mume wake na watoto wake akabaki peke yake, akihisi huzuni kuu na kupoteza familia. Shambulizi la Uchungu wa Nafsi: Alijiona “bila maana” na akajiita “Mara” (kwa maana ya “bitterness ” / Uchungu) akiona maisha yake yametoweka (Ruthu 1:20-21). Shambulizi la Msimu wa Uamuzi: Kurudi Bethlehemu akiwa maskini, bila matokeo yanayojulikana, akibeba hofu ya maisha mapya. ➡️ Orpa Shambulizi la Mauti ,Upweke na hakupata watoto ni pamoja Hatari, Kutojua hatma yake baada ya kifo cha mume wake alibaki kama mgeni bila familia. Shambulizi la Uchungu wa Nafsi Uchungu wa kuachwa peke yako na Naomi; kuhisi mahusiano yametoweka. Shambulizi la Msimu wa Uamuzi; Aliamua kurudi kwa familia yake Moabu, chaguo salama lakini yenye maumivu ya kihisia. ➡️ Ruthu Shambulizi la Mauti, Upweke kwa kukosa wana Hatua ya kuambatana Naomi na kuondoka kutoka nyumbani kwake Moabu inayopelekea hatari ya maisha yasiyojulikana. Shambulizi la Uchungu wa Nafsi Kuachwa nyumbani, kushughulikia hali ya upweke na changamoto ya kuishi kama mgeni katika jamii mpya. Shambulizi la Msimu wa Uamuzi Kuamua kushikamana na Naomi kwa uaminifu wa dhahiri, kumfuata na kumchagua Mungu wa Naomi, badala ya kurudi kwa usalama kama Orpa. AGENDA ZA MAOMBI SIKU YA 2 MAFUNGO YA KWARESMA SIKU 40 1️. OMBA TOBA PALE ULIPOKUBALI KWENDA NA MSIMU BADALA YA KUSUDI KWASABABU NYINGI. 2️. OMBEA AKILI (NIA) YAKO ILI KUKABILIANA NA SHAMBULIZI LA MSIMU KWENYE KUSUDI LAKO ILI KUBAKIA KWENYE KUSUDI NA SIO KUYUMBISHWA NA MSIMU. 3️. OMBEA MAAMUZI YA NAOMI WAKO, MAANA KUNA WAKINA NAOMI WANAVURUGWA NA MSIMU KIASI WASIELEWE WAMEBEBA NINI CHA KWAKO. 4️. OMBA MSAADA WA MUNGU NA DAMU YA YESU ILI KUBATILISHA KILA SHAMBULIZI LA MSIMU LINALOSHAMBULIA KUSUDI LAKO MFANO; MAUTI, UTASA, UCHUNGU (MAUMIVU YA NDANI), KUPOTEZA, UPWEKE N.K Mhubiri: Mwl Renald Mlawi Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com