У нас вы можете посмотреть бесплатно Salama Na MARDHIYA SE6 EP47 | HIARI... PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Salum Mardhiya ni mmoja ya watu maarufu sana kwenye visiwa vya marashi ya karafuu yaani kule kwetu Zanzibar. Ni mmoja ya waalimu hodari anayeongoza kwa kutoa Da’wa kwa watu ambao wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali. Kwenye nyumba karibu zote wanamfahamu maana huonekana mara kwa mara kwenye maeneo mbali mbali ili kusaidia wale ambao wanahitaji kisomo chake. Binafsi nilifahamiana nae kupitia rafiki ambae alinitambulisha kwake mapema mwaka huu, tena haikua imepangwa wala, alikuja sehemu ambayo mie nilikuwepo kuja kupata chai na mimi bahati nzuri nilikua maeneo hayo so mtu akatutambulisha, na akaambiwa kama Mama yangu ni mgonjwa yuko hospitali na yeye akasema basi atakuja baadae kwaajili ya kumuombea dua, na jioni akatokea. Oh kama angependa kujua hali ya Mama yangu Alhamdulillah yuko vizuri. Tunamshkuru Mungu. Kwa mujibu wa story za hapa na pale niliambiwa nilikua na bahati sana kumpata maana ratiba yake ya kutoa Da’wa ni tight sana na watu ni wengi wanaohitaji huduma zake ila muda anakua hautoshi wa kumtilia Dua kila mtu ingawa angependa kufanya hivyo, kwahiyo ilikua kama bahati sisi kukutana na kuanzia hapo tukaanza kuwa tunaonana kwa kiasi. Nikaona si vibaya kama nitamleta kwenye meza yetu ili na sisi tuweze kumfahamu zaidi. Wakati namuambia kuhusu mualiko wa kuja kwenye kiti chetu chakavu hakua na hiyana, aliangalia ratiba yake na akaniambia hiyo tarehe atakuwepo nchini. Sheikh Mardhiya yeye huwa anasafiri sana, Da’wa zake huzitoa sehemu tofauti tofauti duniani, mara nyingi anakua zake Arabuni, mitaa ya Oman na Dubai na Abu Dhabi huwepo sana, kashatibu watu wa aina tele kwenye maisha yake. Kuanzia marajiri mpaka maskini, ambao walikua na imani na anachofanya na ambao hawakua na imani nae. Simu yake huita mara kwa mara na hiyo ni moja ya sababu za yeye kuwa na namba zaidi ya moja na kuwa na wasaidizi kadhaa. So huku kwenye kutoa Da’wa alifikaje? Hii ilikua ndo mwanzo wa maongezi yetu haya. Akiwa kama kijana ambaye angeweza pengine kufanya kazi ya aina yoyote na kujipatia rizki yake, kwanini alichagua hii? Kaniambia tokea akiwa na umri wa miaka sita, alianza kupata upeo huo, bila hata yeye mwenyewe kujua ni nini hasa kilikua kinaendelea katika maisha yake, anakumbuka pia jinsi alivyokua anazimia na kupata uwezo wa kuwasomea walokua wanahitaji kisomo chake na wanakua poa kabisa, anasema hata hakumbuki alikua anawasomea nini baadhi yao ila sasa baada ya kuwa mtu mzima na kupata kuijua vizuri Quran Tukufu ndo anang’amua nini alikua anawasomea watu ule. Mwanzo nilisema Mardhiya ni kijana kwahiyo kwa kiasi kikubwa ana style ya maisha ambayo vijana wengi wangependa kuwa nayo ila uwezo nayo hawana. Kama kuwa na maisha ya kifahari, magari mazuri na mke zaidi ya mmoja, pesa nyingi na nyumba nzuri zaidi ya moja na kusafiri mara kwa mara. Hii kwa ki aina flani imekua ikileta maneno na maswali kuhusu uhalali wa ambacho anafanya au ambacho amekua akifanya. Je maneno hayo yanamzui yeye kufanya ambacho anafanya kwa watu wenye uhitaji? Au kubadilisha aina ya maisha ambayo anaishi? Tumeongea kuhusu masuala ya Husda na wivu, usafi na mmoja kuamua kujipenda zaidi. Je kuna makosa kwenye baadhi ya matamanio ya nafsi zetu? Vipi kuhusu Sadaka? Inatakiwa itolewe ki namna gani? Ipi ni sawa na ipi si sawa? Ipi ni dhambi na ipi ni nzuri ili kuweza kuwafanya na wengine watamani kutoa? Vipi kuhusu Heshima kwa kila mmoja? Wazazi? Nafasi ya Wanawake? Kuhusu imani na uchawi kwa ambacho yeye anafanya? Mmoja anaweza kujuaje kama hii ni kufuru na hii ni sawa? Maswali yalikua mengi na majibu pia yalikua yanatoka kutokana na swali lilivyo ulizwa, yangu matumaini elimu ambayo Mimi nimeipata na kwako itakua vivyo hivyo. Tafadhali Enjoy, Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible &... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz