У нас вы можете посмотреть бесплатно “YAS YATOA TIBA ZA MACHO BURE DODOMA KUPITIA KAMBI MAALUM YA AFYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#dodomafmradio #kapukubwa #ipokwaajiliyako Akizungumza na Dodoma TV, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kati, Said Iddy, amesema kuwa leo ni siku muhimu kwa kampuni hiyo, kwani mbali na kutoa huduma za kimtandao, wameamua kwenda moja kwa moja kugusa maisha ya wananchi kwa kutoa huduma za afya ya macho, jambo linalosaidia kupunguza changamoto za kiuchumi kwa wananchi wenye kipato cha chini. Aidha, Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa zoezi hilo si la mara ya kwanza, kwani kampuni ya Yas imekuwa ikitoa huduma hizo katika maeneo mbalimbali nchini tangu mwaka 2024, na kufanikiwa kuwahudumia wagonjwa zaidi ya elfu thelathini na tano. Kwa upande wake, Mratibu Msaidizi wa Kambi za Macho kutoka Bilal Muslim Mission, Hassan Dinya, amesema kuwa kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine, muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa, ambapo katika siku ya leo pekee wamefanikiwa kupokea na kuhudumia takribani wananchi 600. Nao wananchi wa Jiji la Dodoma wameishukuru serikali pamoja na kampuni ya Yas kwa kuwajali wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ya macho, wakisema huduma hiyo imewasaidia kugundua matatizo ya macho mapema na kupata tiba stahiki Wananchi wameomba kambi hizo ziendelee kufanyika mara kwa mara na kufikishwa hadi maeneo ya vijijini ili kuwafikia watu wengi zaidi. WATCH DODOMA TV📺 STAR TIMES - 113 || DODOMA CABLE 102 || MANENO CABLE - 18 Copyright © 2022 Dodoma Media Group. All Rights Reserved.