У нас вы можете посмотреть бесплатно Mama asimulia watu wasiojulikana walivyompora mwanawe mwenye ualbino, baba wa mtoto awekwa kizuizini или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkazi wa Kitongoji cha Mbale Kijiji cha Bulamula wilayani Muleba mkoani Kagera, Judith Richard (20) amesimulia jinsi watu wasiyojulikana walivyompora mtoto wake mwenye ualbino na kutokomea naye kusikojulikana. Tukio la mtoto huyo wa kike, Asimwe Novath (2) kukwapuliwa mikononi mwa mama yake mzazi na watu hao lilitokea Alhamisi Mei 30, 2024, Saa 1 jioni huku msako wa kumtafuta mtoto huyo na waliomchukua ukiendelea. Mwananchi imefika hadi inapoishi familia hiyo na kukuta ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamekusanyika huku nyuso zao zikitawaliwa na huzuni. Kwa mbali Judith anaonekana katika nyumba ya Tembe akiwa mwenye mawazo, uso wake ukibubujikwa machozi. Akizungumza kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Yusuph Daniel amesema wanamshikilia baba wa mtoto huyo, Novath Asimwe (24) na wenzake wawili wakidaiwa kuhusika.