У нас вы можете посмотреть бесплатно KUKOROTA/KUPUMUA KIFUA KINATOA MLIO: Kujitibu mwenyewe nyumbani или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DR.MNIKO #MNIKO #DR.MNIKO Kukorota ni hali ya kutoa mlio kama mluzi wakati hewa inapopenya kupita kwenye njia ya hewa ambayo ikuwa finyu sana. Ni kama vile unapopuliza filimbi, kama filimbi ni nyembamba sana , mlio wake unakuwa mkali zaidi. Mara nyingi mlio huu utausikia vizuri zaidi mtu anapumua hewa kwenda nje, ila hata anapovuta hewa unaweza kuusikia. Mara nyingi kukorota kutokana na mirija ya kupitisha hewa iliyo ndani ya kifua. Mara nyingi utakuta kuwa kipenyo cha hii mirija inayopitisha hewa kinapungua au kufinywa kwa sababu ya maambukizi ya virusi au aleji kama ilivyo kwa watu wenye ugonjwa wa pumu. Kwa watoto wenye umri chini ya miaka 2, mifereji ya hewa midogo zaidi inaweza kufinywa kwa sababu tu ya maambuzki ya virusi. Kuwa na ugonjwa wa pneumonia unaweza pia kusababisha mkoroto. Kwa mara chache, utakuta labda kuna kitu alichomeza kwa bahati mbaya kimeziba sehemu ya mfereji wa njia ya hewa na kusababisha mkoroto – aina hii ya mkoroto inaweza kuwa ngumu kusikia isipokuwa kwa kutumia kifaa maalumu cha daktari “stethoscope” Kwa watu wanovuta sigara, usumbufu unaosababishwa na msohi wa sigara kwenye mifereji ya njia ya hewa, unatosha kabisa kusababisha mfereji kuwa finyu na hivyo kusababisha mkoroto. Kama utakuwa na ugonjwa wa pumu pia, itasababisha hali kuwa mbaya zaidi. Ugonjwa wa pumu Ugonjwa pumu ni ugonjwa unaowapata zaidi watoto na vijana walio kwenye balehe. Ni ugonjwa unaongezeka siku hizi. Mkoroto unaompata mgonjwa wa pumu, unatokana na kukaza kwa misuli ya mfereji wa njia ya hewa na hivyo kupunguza kipenyo cha mfereji wa hewa, hii inasababisha ugumu kwa hewa kupita na hivyo kusababisha mkoroto. Kwa sababu aleji ndio husababisha tukio la pumu, utando ute wa mfereji wa hewa unatengeneza uteute mwingi kama kamasi ambao pia unachangia sana katika kupungua kwa kipenyo cha mfereji wa hewa na kuongeza tatizo la kupumua. Unaweza kupata tatizo la kubanwa na pumu kwa sababu ya maambukizi, hisia kali zinazotokana na kuudhiwa na kitu, hali ya hewa ya baridi, uchafuzi wa hewa kama vumbi nyingi au kukutana na chavua za maua ya mimea. Baadhi ya vitu vinavyoweza kusababisha ukabanwa na pumu ni pamoja na vumbi, chavua za maua ya mimea, kuvu, aina Fulani za vyakula ulivyonavyo aleji na manyoya ya wanyama. Unaweza pia kupata mkoroto baada ya kuumwa na mdudu Fulani au baada ya kutumia dawa; mfano, wapo watu wanaokorota baada ya kumeza dawa ya Asprin. Il kiukweli, mara nyingi kwa watu wengi huwa sababu ya kupata tukio la kubanwa na pumu haijulikani. Unapokorota na una homa Kwa mtoto mwenye maambukzi kwenye mfumo wa hewa, anaweza kuanza kukorota kabla hajaanza kupata shida kupumua. Kwa hiyo, kama ana korota na ana homa pia – hii inaweza kuwa dalili ya maambukizi – nenda kaonane na daktari mapema. Mambo yafuatayo nitakayozungumza hapa, unaweza kuyafanya ukiwa nyumbani, hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa msaada wa daktari ni muhimu. Ni daktari pekee anayeweza kukupatia dawa ya kupanua mfereji wa dawa ambao umekuwa finyu ili upumue vizuri. Anaweza pia akakuongezea maji mwilini kupitia kwenye mshipa ili upone haraka zaidi. Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama una korota Mtoto yoyote anayekoroata natakiwa kuonana na daktari mapema, hasa kwa mara kadhaa za mwanzo. Ugonjwa wa pumu unatokea kwenye familia, utakuta wapo watu wengine kweny familia wenye pumu, pumu ya ngozi na aleji nyingine. Kunywa maji ya kutosha ni muhimu, ila unaweza kunywa hata juisi au hata kinywaji baridi kama itasaidia unywe maji mwengi zaidi. Kunywa maji ni sehemu ya tiba hata ukifika hospitalini, kwa hiyo ni vyema ukaanza kunywa maji ukiwa nyumbani. Unaweza kutumia vaporizer ili kuvuta mvuke wake, kama hauna vaporizer unaweza kuweka maji ya moto kwenye bakuli, ukakiinia kibali hicho, chukua kitambaa ufunike kichwa kisha vuta mvuke wake, JIFUKIZE, itakusaidia kujihisi vizuri. Hakikisha mazingiria unapokaa hakuna vumbi. Hakikisha unasafisha kapeti, masofa, na kufua matandiko yote mara kwa mara. Kwa watoto, hakikisha midoli ya kuchezea ni safi; ni vizuri ukanunua midoli inayoiweza kufuliwa. Kama unatumia air conditioner, hakikisha unasafisha au kubadilisha chujio/filter zake mara kwa mara. Kama una ugonjwa wa pumu, daktari atakupatia maelezo zaidi na kukupatia dawa za kutumia unapobanwa kifua kwa sababu ya pumu.