У нас вы можете посмотреть бесплатно EPUKA SIFA NA MANENO YASIYOKUJENGA: Tafuta Mafanikio ya Kweli | LENZI | Michael Kamukulu или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Epuka sana maneno na sifa nyingi ambazo hazikupi faida wala kukuletea mafanikio hata kama zinatoka kwa marafiki. *** Njaa hutibiwa na chakula, wala sio harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. *** Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi yatakayotupa kufanikiwa kwenye kazi, kukuza faida kwenye biashara, kuongeza wigo kama viongozi / kiongozi, kuboresha mahusiano ndani na nje ya ndoa pamoja na mambo mengine mengi. Mojawapo ya njia za kuongeza mafanikio yanayotokana na maamuzi yetu ni kujitambua, kuweka malengo na kuwa na uwezo wa kuyapima malengo kwa kipimo sahihi. Zipo siri na kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kila mtu, lakini walio wengi wamechagua hisia kuliko uhalisia. Watu wengi hupima mafanikio ya maamuzi yao katika maisha, biashara, mahusiano hata kazi kwa kuangalia ni kwa kiasi jamii ikiyowazunguka inaridhishwa. Hata kama itahusisha maumivu, hasara au majuto, bado watu walio wengi wako tayari kufanya jambo wasilolitaka ilimradi wengine wawakubali na kuwaheshimu. Si mara zote matokeo yanakuwa chanya, na ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia faida zote, binafsi na zile za jumla ili matokeo ya maamuzi yoyote yale yasije yakaishia kuwa majuto, hasira, chuki, aibu ama kukata tamaa. * * Hadithi/Simulizi Mtoto (yatima) aliomba chakula cha kwake na wadogo zake ili wasife njaa baada ya kukaa siku nyingi bila mlo wowote. Mtu mzima aliyeombwa chakula alimjibu kwa kutoa ushauri, “chukua kitunguu swaumu ukakichome kwenye moto, majirani wakisikia watasema mmepika na kuka chakula kizuri”. Huu ushauri haukulenga kutatua tatizo halisia, ulilenga kuionesha jamii kwamba hakuna tatizo wakati huo huo madhara yakiendelea kutokea kwa watoto. * * Ongeza uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia njia bora ambazo hazina madhara. Sikiliza uweze kujifunza zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI | @lenzi.michaelkamukulu