У нас вы можете посмотреть бесплатно Walichokisema Mawakili, Wananchi Baada ya Mahakama Kubariki TAMISEMI Kusimamia Uchaguzi или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam imehalalisha Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa kufuatia wananchi watatu kuwasilisha kesi ya kupinga wizara hiyo kusimamia uchaguzi huu. Katika hukumu iliyosomwa leo Oktoba 28, 2024, na Jaji David Ngunyale, mahakama imesema kuwa Waziri wa TAMISEMI ana mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Na katika hoja iliyowasilishwa kuwa Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo yenye wajibu wa kusimamia uchaguzi huo mahakama imesema kuwa tume hiyo itasimamia endapo kutakuwa na sheria rasmi itakayotungwa na kuipa jukumu hilo. Baada ya kutolewa kwa maamuzi hayo wananchi waliowasilisha kesi hiyo wameeleza kuhusu mpango wao wa kukata rufaa, lakini kwa sasa wamewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye michakato yote inayoendelea ya uchaguzi huo. Unaweza kutufuatilia kupitia; TWITTER: / thechanzo INSTAGRAM: / thechanzo FACEBOOK: / thechanzo TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_... Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105 The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.