У нас вы можете посмотреть бесплатно DKT. TULIA: HAKUNA KIUMBE KINAWEZA KUSHINDANA NA DKT. SAMIA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, leo Septemba 17, 2025 amezindua rasmi kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ikungi Magharibi, mkoani Singida, na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Elibariki Kingu. Akihutubia katika mkutano wa Kampeni uliofanyika Kata ya Sepuka, Dkt. Tulia ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, amesema kwa sasa haoni mtu yeyote nchini Tanzania mwenye uwezo wa kushindana na Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo ya Uongozi. "Kuna watu waliojitokeza wakisema nao wana jambo la kuwaambia wananchi, lakini jambo la dhahiri ni kwamba hakuna kiumbe yeyote kwa sasa ndani ya nchi anayeweza kushindana na Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Dkt. Tulia. Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu, alibainisha kuwa maendeleo makubwa yaliyotekelezwa katika kipindi kilichopita ndiyo msingi wa kukubalika kwake kwa wananchi. Aliongeza kuwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake ni ushahidi kwamba wanajitokeza kwa hiari bila kushinikizwa wala kupewa hongo.