У нас вы можете посмотреть бесплатно MBUNGE ATEKELEZA AHADI YA ZAWADI KWA KILA ONE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Furaha kwa nafunzi na wahitimu kyela Mbunge wa Jimbo la Kyela, Baraka Mwamengo, ametekeleza ahadi yake kwa kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wa Wilaya ya Kyela waliohitimu kidato cha nne na kufaulu kwa kupata Division A katika somo la hesabu. Katika hafla hiyo, mbunge huyo alikabidhi kiasi cha shilingi 100,000 kwa kila mwanafunzi aliyefanya vizuri kama motisha ya kuhamasisha juhudi na kuongeza ari ya kufanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi. Hatua hiyo imelenga kuhamasisha wanafunzi wengine kupenda na kufanya vizuri katika somo la hesabu pamoja na kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya ya Kyela. Sambamba na tukio hilo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makwale wamewasilisha ombi kwa mbunge huyo la kusaidiwa ujenzi wa bweni la wanafunzi, wakiamini kuwa miundombinu bora ya malazi itasaidia kuongeza umakini katika masomo na kuboresha zaidi ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.