У нас вы можете посмотреть бесплатно #TAZAMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
SERIKALI imetoa kibali Kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukopa kiasi cha sh.bilion 173.9 kwa ajili ya kukwamua miradi iliyokwama katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Allan Kijazi kwa amesema kwa kuanzia tayari Shirika limeidhinishiwa na hazina mkopo wa shilingi bilion 44.7 ili kuendelea kazi ya kuifufua miradi hiyo. Dk.Kijazi ametaja miradi iliyokwama kuwa ni pamoja na mradi wa Kawe 711, Morocco Square na mradi wa Plot 300 regent Estate iliyopo Dar es salaam. Kuhusu mradi wa nyumba 1,000 unaotekelezwa na NHC Dodoma Dk.Kijazo amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ilitoa mkopo nafuu wa sh. bilion 20 Kwa shirika ili zitumike kama mtaji ambao utatekelezwa Kwa Miaka 15. Amesema mkopo huo utalipwa kwa miaka 12 baada ujenzi wa mradi wa nyumba 1,000 kukamilika ambapo adhma ya serikali ni kuwezesha Shirika kujenga nyumba Dodoma ili kurahisisha upatikanaji wa makazi baada ya serikali kuhamishia shughuli zake. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dk. Maulid Banyani amesema shirika liliendesha operesheni maalumu Kwa wadaiwa sugu ambapo ilisaidia Shirika kukusanya sh. bilion 5 kati ya 27 inazodai kutoka Kwa wateja wake. Amesema operesheni hiyo itakuwa endelevu na sasa wanakuja na mfumo maalumu ambao utakusanya kodi kwa njia ya kisasa na mfumo huo upo katika majaribio katika nyumba za chamwino. Kuhusu mradi wa Kawe 711 Dk. Banyani alisema tayari mkandarasi yuko saiti anaendelea na kazi ndogo ndogo. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo: / spotileo-176. . HabariLeo: / habarileo DailyNews: / dailynewstz INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09