У нас вы можете посмотреть бесплатно MGOGORO MKUBWA WAIBUKA KKKT FOREST MBEYA | VIONGOZI WANNE WA KWAYA KUU WASIMAMISHWA, GARI LIKITAJWA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Usharika wa Forest jijini Mbeya wamesema hawakubaliani na uamuzi wa kanisa hilo kufuta Kwaya Kuu na uongozi, wakiahidi kesho kuingia kanisani kufunga muziki ili wafukuzwe. Mgogoro huo umeibuka baada ya kanisa kupinga uamuzi wa kusimamishwa kwa baadhi ya viongozi na Kwaya Kuu huku ikielezwa kuwa Novemba 2024, Dayosisi ya Konde ilituma waraka uliotaka idadi ya kwaya zipungue kutoka kwaya tano hadi kwaya tatu. Hata hivyo, ingawa kwaya zilizopendekezwa kufutwa zilikuwa Safina na Hosiana, viongozi wa usharika huo wameamua kuifuta Kwaya Kuu badala yake na wanakwaya kutakiwa kujisajili upya. Awali, usharika huo ulikuwa na kwaya tano ambazo ni Kwaya Kuu Forest, Kwaya ya Uinjilisti, Kwaya ya Hosiana, Kwaya ya Safina, Kwaya ya Vijana na Kwaya ya Uwaki. Baadhi ya waumini wakizungumza nje ya Kanisa hilo hii leo Agosti 30, 2025 wamesema hawakubaliani na hatua hiyo, wakisisitiza kuwa Kwaya Kuu ina historia ya zaidi ya miaka 45. Katibu wa Kwaya Kuu, Julius Mwaikusi, amesema barua ya Dayosisi ilielekeza kupunguza kwaya, lakini utekelezaji wake umeleta sintofahamu, "Lakini imeenda mbali wakadai tusimamishwe kazi ikiwa ni Mwaikusi, Yonah Mwaisango, Michael Mwangonji na Petro Kyando na hakuna sababu ya kusimamishwa kwao." Alisema Mwaikusi Naye mwalimu wa Kwaya Kuu, Yonah Mwaisango, amebainisha kuwa chanzo cha mgogoro huenda ni baada ya Kwaya Kuu kununua gari jipya. Amesema licha ya wao kufuatilia suala hilo kwa viongozi wa kanisa, bado hawajapatiwa majibu. Kwa upande wake Rehema Ibanje ambaye ni Makamu Katibu wa Kwaya Kuu amesema hatua ya viongozi wa kanisa hilo kutaka mali za Kwaya Kuu zikabidhiwe kwa Halmashauri kuu ya Kanisa haiingii akilini kwa kuwa mali hizo ni michango ya wanakwaya wenyewe, "Zaidi wanatuambia mali za Kwaya Kuu zikabidhiwe kwa Halmshauri hali ambayo ni tofauti kwa kuwa hakuna mchango wowote wa mtu zaidi ya sisi, tulichogundua ni kwamba wanataka kuwapa wengine na hatukubali," alisema Bi Rehema. Hata hivyo Manara Tv imefanikiwa kuzungumza na Mkuu wa Jimbo la Mbeya Magharibi Mchungaji Lusajano Sanga kwa njia ya Simu ambapo amesema hajafahamu kinachoendelea, "Sijajua kinachoendelea, sijaambiwa chochote na mchungaji ili aniambie kama kuna tatizo nijue tutafanyaje." ✍🏼 @ndambo_17