У нас вы можете посмотреть бесплатно IBADA YA TAREHE 25.01.2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MAHALI: TAG MULEBA SOMO: MAOMBI Ujumbe wa Somo: Katika somo la leo la Maombi, mchungaji aliwakumbusha wapendwa kwamba maombi ni pumzi ya maisha ya Mkristo. Hakuna Mkristo anayeweza kuishi maisha yenye ushindi bila kuwa na maisha ya maombi. Maombi humunganisha mwanadamu na Mungu wake, humfanya Mkristo kusikia sauti ya Mungu na kupokea mwelekeo sahihi wa maisha. Aliwasisitiza wapendwa kwamba maisha bila maombi ni hasara kubwa akitolea mfano wa samaki na maji samaki bila maji haina maisha, kwa sababu bila maombi tunakuwa dhaifu kiroho, tunakosa ulinzi wa Mungu, na tunapoteza ushindi ambao Mungu ametupangia. Maombi si chaguo, bali ni hitaji la kila siku kwa mtoto wa Mungu. Uhusiano na Mfungo wa Siku 21: Mchungaji aliwakumbusha kuwa kwa sasa makanisa yote ya TAG yako katika mfungo wa siku 21, hivyo huu ni wakati wa pekee wa kujitoa zaidi katika maombi, kufunga na kumtafuta Mungu kwa bidii. Aliwahimiza waumini wasikae nyuma, bali washiriki kikamilifu, wakitumia muda huu kujenga mahusiano yao na Mungu kupitia maombi ya dhati.