У нас вы можете посмотреть бесплатно Salama Na LULU DIVA SE6 EP61 | UKIPATA KINYAKUE… PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Kuna mambo mengi wakati mwengine ambayo yanakua yanaendelea au yalitokea kwenye maisha ya baadhi ya watu ambao huja kukaa kwenye kiti chetu chakavu na meza yenye kigae. Ila kwasababu zilizo wazi za kuwataka wasijisikie uncomfortable na pengine kuwafanya hata ambao wangependa au ambao tungependa waje nao wasijiskie hivyo ndo kanuni ambayo tumeamua au niseme niliamua kipindi huko nyuma kuifuata. Nia na madhumuni ya session zetu hizi zaidi ni kuwapa watu maua yao wakiwa hai, sisi nasi kuskiliza hadithi za maisha yao ambazo zitatupeleka sehemu fulani katika maisha yatu na hili pia humuambia kila mgeni anapokalia tu kiti chetu chakavu kabla hata camera hajiwashwa ya kwamba… Sisi tuko hapa kwaajili ya kutaka ku inspire zaidi na si kumdhalilisha au kutaka kumuangalia kwa chini yoyote kwasababu tu kabla kuna kwikwi kadhaa zilishawahi kutokea kwenye maisha yake na tuka tumia hiyo kama ‘fimbo’ kumchapia nayo. Kama mwenyewe ana simulizi yake ya ‘majuto’ ambayo wengi wanaifahamu na haikumueka sehemu nzuri na angependa kuiongelea basi ruhusa ipo, ila kama ni kitu ambacho mwenyewe hayuko tayari kukiongelea basi kuheshimu hilo ni jukumu letu NAMBARI MOJA. Najua pengine inawezakana kabisa ukaona ah basi kuna haja gani ya kuongea nao then? Haja ipo na naamini tukipatacho hutosha, bila ya kuvunjiana heshima au kuwekana uncomfortable. Ukikua zaidi utaelewa zaidi . Lulu Diva ni moja ya majina makubwa kwenye muziki wetu hapa nyumbani na pia kwenye kiwanda cha uigizaji, hustle zake za spidi KUBWA ndo ambazo zimemfanya awe anatambulika na mambo mengine kuweza kwenda vizuri kama jahazi kwenye hali ya hewa shwari huko baharini. Ila hayo yote hayakuja tu kwasababu labda yeye ni maalum sana, au mzuri sana au anajua kuimba sana, kiukweli wake, haya yamekuja baada ya jasho tele, mchozi tele na pengine damu kiduchu. Jinsi alivyokua ilikua kwa malezi ya Bibi maana Mzee wake alikua na mambo mengi, Mama yake nae alikua akimpambania goli kama wengi ambavyo wamekua wakifanya kwa watoto wao. Kukua kwake kwa kiasi kikubwa ni Tanga na ananisimulia kwenye apisode hii jinsi ambavyo alikua akihama vijumba na maamuzi magumu ambayo aliyafanya yeye na Marehemu Mama yake ya yeye kuja TOWN. Lulu ananihadithia pia jinsi alivyokua akijituma ili aweza kumleta Mama yake mjini baada ya kuskia ameanguka kwa mara ya kwanza. Ni binti tu ambaye ndoto yake ilikua ni kuishi na Mama yake mzazi ambaye maisha hayakua hivyo wakati anakua. Ilikua inambidi afanye mambo kadhaa mpaka alipoweza kutimiza ndoto yake hiyo ya kumleta Bi Mkubwa hospitali kwa mara ya kwanza. Mengi yalitokea na ambayo yalikua nje ya uwezo wake ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu kadhaa aliweza kuyakamilisha ambayo kwa mujibu wa simulizi zake naamini Mama ametangulia mbele ya Haki akiwa na roho safi kwa Binti yake. Story ya Mama Lulu ndo ambayo kwa kiasi kikubwa ilibeba mazungumzo yetu haya, ingawa pia kwa ki upekee kabisa tumeweza kuzungumzia mahusiano yake, kazi zake, ndugu zake, maisha nyuma ya camera , kazi zake, uandishi, muziki na filamu na hakua mchoyo wa kujielezea na kutuelezea hata kidogo. Yangu matumaini pia nawe utaskiliza na kuitimaza kwa MAKINI na kwa kiasi fulani utaweza kuelewa baadhi ya mambo ambayo yatakufanya hata ukimuona uwe na heshima fulani kwa Binti huyu. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible &... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz