У нас вы можете посмотреть бесплатно DARAJA LA KINYEREZI-BONYOKWA LAKATIKA, WAKAZI WASOTA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wakazi wa Bonyokwa, jijini Dar es Salaam, wanakabiliwa na changamoto ya usafiri baada ya daraja linalounganisha Bonyokwa na Kinyerezi kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Hali hiyo imeathiri shughuli za kila siku, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kushindwa kwenda shule na wafanyakazi kuchelewa kazini. Mkazi wa Bonyokwa, Sara Philimon amesema kukatika daraja hilo kumeathiri maisha yao kwani wanashindwa kuvuka kwenda kwenye shughuli zao za kila siku. "Sijakwenda kazini leo kwa sababu daraja limekatika. Siyo mimi pekee, hata wanafunzi wameshindwa kwenda shule. Wengine wanalazimika kupelekwa na wazazi wao kwa kutumia njia zingine za kuzunguka. Tunaomba Serikali itusaidie kurudisha hali ya kawaida, kwa kuwa tunateseka," amesema Sara. Mkazi wa Bonyokwa Kisiwani, Samaduni Mlimbwa amesema kuwa walishatoa ushauri kwa mkandarasi kabla ya kujengwa kwa daraja la muda, lakini ushauri wao haukuzingatiwa. "Tulieleza kuwa daraja la muda wanaloweka halitaweza kusaidia kwa sababu maji yanapita kwa wingi na njia waliyoweka ni ndogo. Pia, mvua mara nyingi huja na takataka kama miti na majani. Lakini hawakutusikiliza, na sasa hali ndiyo hii," amesema Mlimbwa. Ameongeza kuwa wao kama wananchi wanapenda maendeleo, lakini kuondolewa kwa daraja la awali na kuwekwa daraja la muda katika kipindi cha masika haikuwa uamuzi sahihi.