У нас вы можете посмотреть бесплатно AGIZO LA RAIS WILAYANI BUNDA HALIJATEKELEZWA FAMILIA ZAIDI YA 10 WAMLILIA RAIS SAMIA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
“Kutokea mkoani Mara wilayani Bunda, moja ya maeneo ambayo baadhi ya wananchi wamejitokeza leo, wakiomba hatua za haraka kwa ndugu na vijana wao wanaoshikiliwa kufuatia madai ya kushiriki maandamano ya Oktoba 29 na 30 kuachiliwa huru. Haya yanajiri baada ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia na kufungua Bunge la 13 alipoagiza DPP muendesha mashtaka mkuu wa Serikali kuchukua hatua za kuchuja baadhi ya makosa na kuachia wale waliokamatwa wakati wa maandamano ya tarehe 29 na 30 huku akidai wengi wao walifata mkumbo na hawakujua walitendalo. Kwa upande wa bunda agizo hilo la Mhe. Rais inadaiwa kutotekelezeka hata kwa mtu mmoja kuachiliwa huru jambo linalozua maswali mengi kwa wakazi wa bunda huku familia za ndugu hao zikihoji Bunda kuna nini mbona sivyo kama agizo la rais lilivyotekelezeka katika wilaya zingine na mikoa mingine. Familia hizo zikielekeza kilio chao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedai kuwepo kwa changamoto za kuwaona ndugu zao pindi wanapowatembelea gerezani na pale wanapofika mahakamani kwaajili ya kufuatilia shauri hilo tangu lilipoanza kutajwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda ndugu zao hawafikishwi mahakamani kwasababu ambazo wadai wanadai hazina mshiko ikiwemo kukutana na majibu ya kama "upungufu wa maaskari wa kuwaleta mahakani". Jambo Tv tuliwatafuta mawakili wa kujitolea upande wa watetezi ambao nao kwa upande wao wameeleza juu ya shauri hilo namba "Preliminary Inquiry Case Namba 26596/2025" bila kuingilia mahakama wakisema kwa upande wa bunda watu 30 wanashikiliwa kufuatia vurugu za maandamano na mpaka hakuna hata mmoja ambaye jamhuri imemuachia iwe kwa kufuatia agizo la Rais au vinginevyo, wamesisitiza wao kama mawakili wataendelea kufuatilia na kusimamia shauri kila litakapokuwa linatajwa mahakamani hapo sambamba na kuwatembelea watuhumiwa mahabusu. Jambo Tv hatukishia hapo tulimtafuta mwendesha mashitaka wa Serikali wilayani Bunda Afande Athuman kwa njia ya simu mwenye namba inayoishia 004 bila mafanikio huku simu yake ikiita mara kadhaa bila kupokelewa na wakati mwingine kutumika pamoja na kumuachia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) lakini jitihada hizo za awali hazijazaa matunda lakini bado tunaendelea kuwekeza muda kumtafuta. Swali linaloibuka ni — nini kinaendelea? Na ni kwa nini baadhi ya wananchi hapa wilayani Bunda bado hawajapata majibu, mpaka kufikia hatua ya kutafuta huruma mpya ya Rais? Inaelezwa kuwa miongoni mwa Waliokamatwa wapo wanafunzi wa secondary ambao mara kadhaa wamekuwa wakifikishwa mahakamani na kesi kupigwa tarehe mara kwa mara huku ikidaiwa uchunguzi haujakamilika. Leo Jambo Tv tunasikiliza sauti zao — si kwa lawama, bali kwa matumaini.” tunakusogezea hali halisi ya vilio vya wananchi hawa. #jambotv #live #askari #ccm #chadema #g55 #jambo #mahakamani #tundulissu