У нас вы можете посмотреть бесплатно VIDEO: KANISA LA FPCT LATOA BATI 130 KITUO CHA POLISI NKINGA IGUNGA, ASKOFU MKUU AKABIDHI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kanisa la The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) linaloongozwa na Askofu Stevie Mulenga Mei 18, 2024 limekabidhi mabati 130 yenye thamani ya zaidi Tzs 4,500,000/= (Milioni nne na laki tano) katika kituo kidogo cha Polisi cha Nkinga kilichopo tarafa ya Manonga wilayani Igunga. Akikabidhi mabati hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo, Askofu mkuu Mulenga amesema, Mwezi Machi, 2024 wakiwa kwenye vikao vya Halmashauri kuu vilivyofanyika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Nkinga walipokea ombi toka kwa mkuu wa kituo cha Polisi juu ya uhitaji wa bati 130 na kuahidi kuwapatia. Askofu mkuu Mulenga amesema kilichomleta Nkinga kwa sasa sio tukio la kukabidhi mabati hayo isipokuwa ni semina ya Pentekoste anayoendelea nayo katika kanisa la Mahali Nkinga kwa Mchungaji Paul Mayengo, na uongozi wa Jimbo la Nzega waliona vema mabati hayo yakabidhiwe kipindi hiki. Aidha, Askofu Mulenga licha ya kukabidhi mabati hayo ameahidi pia kutoa Kompyuta moja na Printa pindi jengo hilo jipya litakapokamilika. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Igunga Mhe.Sauda Mtondoo licha ya kulipongeza kanisa la FPCT kwa mchango walioutoa, pia ameipongeza kamati ya maendeleo ya kata chini ya Mhe.Diwani Samuel Masanja kwa kuibua wazo la ujenzi wa jengo hilo, na kuwaasa wananchi kufanya mambo ya kimaendeleo wao wenyewe bila kusubiri kufanyiwa na serikali, kwani kufanya hivyo kutaharakisha maendeleo. Nae Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amelishukuru kanisa la FPCT kwa kusapoti huduma za kijamii, ambapo amesema mchango uliotolewa haujagusa tu jeshi la Polisi bali hata jamii itakayopata huduma kituoni hapo. Awali mwenyekiti wa kamati ya maendeleo kata ya Nkinga mhe. Diwani Samuel Masanja katika hotuba yake, amesema waliposikia Halmashauri kuu ya kanisa la FPCT inafanyia vikao vyake katika kata ya Nkinga, walijisikia kuheshimiwa na kuthaminika na walijipanga vema katika swala zima la ulinzi na usalama, na waliona vema kuwashirikisha ombi hilo viongozi hao. Ujio wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya kanisa la FPCT katika jimbo la kikanisa Nzega mwezi Machi, 2024 ni utaratibu wa kawaida wa kanisa hilo kufanyika kila mwaka kwa kuzungukia majimbo, vikao hivyo vya Halmashauri kuu vilifanyika ukumbi wa Astrid Boork uliopo eneo la Hospitali ya Rufaa ya Nkinga. Tukio la kukabidhi mabati hayo limeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi toka ndani na nje ya kata ya Nkinga akiwemo mkuu wa idara ya afya taifa kanisa la FPCT na Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Dkt.Tito Chaula.